NA MWANDISHI WETU
MWANAHARAKATI Salma Said amekanusha taarifa
zinazosambaa mitandaoni zikumuhusisha na uhusiano wa kimapenzi na Kiongozi Mkuu
wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.
Akizungumza na TANZANIA PANORAMA jana kuhusu taarifa
za ndoa yake kuvunjika baada ya kufumaniwa na mumewe akiwa na Zitto, alisema
haijavunjika na hana uhusiano naye wala hafahamiani naye.
Salma alisema taarifa zinazo muhusisha kimapenzi na
Zitto aliziona mitandaoni tangu Ijumaa wiki iliyopita lakini alizipuuza kwa
sababu anajua zina lenga kumziba mdomo ili asisimamie anayoyaamini katika
shughuli za kiunaharaka.
Hata hivyo, Salma ambaye pia ni Mwandishi wa habari
alihoji kama maswali anayoulizwa na TANZANIA PANAROMA yanalenga kutumika
kuandika habari na alipoelezwa lengo ni hilo aliomba habari hiyo isiandikwe.
"Wananichafua, Zitto siyo mpenzi Wangu wala
simjui. Sina chama mimi ni mwanaharakati. Wanataka tu kunifunga mdomo lakini
siogopi wala sinyamazi.
"Yaani hata sijui kwanini hawa watu wa
CCM na serikali wananiogopa. Tatizo la Zanzibar ukisema ukweli wanakuita
mpinzani. Lakini mimi nilishazoea kuzushiwa kama unakumbuka hata nikipotekwa
wakati ule walizusha kuwa nilikuwa nimefichwa na bwana mahali.
" Hiyo kitu sisi tuliiona mitandaoni tangu
Ijumaa na nilipoiona tu nilimrushia mume Wangu yeye yupo Dar akaniuliza nani
kaandika nikamwambia apuuze," alisema Salma.
Alipotafutwa Zitto simu yake ilionyesha inatumika
muda wote na alipofatutwa Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Arodia Peter alisema
hana taarifa kuhusu taarifa hizo na kushauri atafutwe Zitto mwenyewe
kulizungimzia suala hilo na kutoa namba ya Zitto inayopatikana.
TANZANIA PANORAMA lilimpigia tena Zitto kwa
namba iliyotolewa na Arodia ambayo pia ilionyesha inatumika muda wote na hata
alipotumiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake hakujibu.
Tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kumekuwa taarifa
zinazodai kuwa Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto amevunja ndoa ya Salma na
kwamba mume wake amehamia jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment