banner

MCHOKONOZI

HISTORIA INAPOANDIKWA UPYA IKILITAMBUA JINA LA TUNDU LISSU

NA CHARLES MULLINDA

KWA mara nyingine, historia ya siasa za Tanzania inaandikwa upya baada ya jina la Tundu Lissu kuchomekwa likiwa limeandikwa kwa wino uliofifia unaoumba maandishi yanayoumiza macho kuyasoma.

Jina la Lissu sasa linasomeka katika  historia ya siasa za Tanzania kuwa ni mwanasiasa aliyerejea nchini akitokea Ubelgiji alikokuwa akiishi baada ya kutibiwa na kupona matobo zaidi ya 10 ya risasi alizomiminiwa na magaidi wa utu wa mtu.

Halijaandikwa katika chapta moja, kuna chapta nyingine inayomuelezea Lissu kuwa mwanasiasa aliyegombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa staili ya kucheza na akili za Watanzania wachache hasa vijana wasiokuwa na mbele wala nyuma ili kutimiza dhamira yake ovu ambayo kwa hakika haikuwa kuwa Rais wa Tanzania, bali kuwa Mtanzania wa kwanza kuwasaidia wazungu kushika vizuri mpini wa kisu kuichinja Tanzania.

Lissu, mwanasiasa mwenye taaluma ya sheria sasa anasomeka katika vitabu vya historia kuwa mwanasheria aliyeitumia elimu yake ya sheria kuzitikisa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuangalia vipengele vya sheria vinavyotoa mwanya wa kuzishambulia moja kwa moja ofisi hizo, na au kuchagua maneno yenye ukakasi ambayo yalikuwa hayamfungi kisheria kuwashambulia washindani wake wakati wa kinyang'anyiro cha kuusaka urais na wakati mwingine vyombo vya dola.

Historia sasa inamtaja Lissu kuwa mwanasiasa aliyefanikiwa sana kwa hila za kisiasa na pia mtu aliyefanikiwa kuwashambuliwa kwa maneno ya hovyo na kwa namna mbaya kabisa viongozi wakuu wa Tanzania pasipo kuchukuliwa hatua zozote kwa sababu siasa ni mchezo mchafu hivyo wanaoucheza wanaruhusiwa kuchafuana.

Anasomwa kwa bidii na watoto na wajukuu zetu kuwa mtu aliyehamasisha vurugu ili nchi iingie katika machafuko na pia mzushi wa kupindukia  aliyethubutu kuzusha uongo wa makusudi kwa watendaji wa serikali pasipo kuchukuliwa hatua yoyote.

Lissu ameandika historia mpya katika taifa letu kwa maneno na matendo yake ya hovyo yenye kila viashiria vya uovu dhidi ya taifa.

Chapta ya mwisho yenye wasifu wake inamwelezea Lissu kuwa ni mwanasiasa mtata, muongo, mjuvi wa sheria, mvurugaji, mtumishi wa wazungu aliyetumwa na mabwana zake kuja kufanya vurugu za kisiasa katika nchi ya baba na mama zake ili wamwage damu na hatimaye taifa liangamie lakini akashindwa kwa hoja zenye mashiko za mwanasiasa asiyecheka na nyani ambaye kwa sababu ya ucha Mungu wake, alimsamehe dhambi zake zinazosameheka.

Historia inapoandikwa upya sasa, inawakumbusha Watanzania kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa zinazoongoza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na NEC ili kuziba mianya kwa watu wa aina ya Lissu kutumia kivuli cha uanasiasa kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

Ili historia itende haki itailazimu kuelezea mafanikio ya uovu wa Lissu yaliyoanza kuonekana mapema baada ya kutoka hospitalini Ubelgiji alikokuwa akitibiwa majeraha ya risasi alizopigwa katika shambulio baya lilitokea jijini Dodoma zaidi ya miaka mitatu iliyopita wakati akitokea bungeni kurejea nyumbani kwake kwa mapumziko ya mchana.

Lissu aliitumia vizuri nafasi hiyo kwa kuanza kuzunguka kwenye nchi mbalimbali za Ulaya na Amerika kuwaomba Watanzania wanaoishi huko pamoja na wazungu wamwangalie kwa jicho la huruma, wamchangie pesa za kujikimu yeye mwenyewe na pia za kuitunza familia yake na kusomesha watoto wake.

kulainisha mioyo ya aliokuwa amewalenga kumpa pesa, Lissu aliishambulia kwa namna ya kuisingizia serikali na vyombo vya dola kuwa ndivyo vilivyomshambulia na kwa sababu waafrika wasiokuwa na akili sawasawa wamejengewa mawazo kuwa staili ya serikali nyingi za wazungu kuwashambulia na hata kuwaua wanasiasa wa upinzani ndiyo inayotumiwa pia na serikali za kiafrika, aliaminika kirahisi. Akajazwa mapesa.

Mbali ya kupita akiombaomba kwa wananchi wa kawaida na taasisi mbalimbali za wazungu, Lissu alipitapita pia kwenye taasisi zinazohubiri na kutekeleza matendo ya dhambi ambazo nazo zilimchangia na alifanya nazo mazungumzo ambayo yanahitaji uwanja mwingine kujadili.

Jambo moja lililobainika katika ziara za Lissu kwenye baadhi ya mataifa ya Ulaya na Amerika kuombaomba ni kuwa, watu wengi, waafrika na wazungu ni bendera fuata upepo na ama huwa hawana muda wa kufikili sawasawa hivyo haikuwa kazi ngumu kwa Lissu kuwaaminisha kile alichotaka yeye waamini.

Hawakuwa na muda wa kujiuliza tangu lini mzungu alimpenda muafrika kwa moyo wa dhati, hawakujiuliza wema wa wazungu kwa Lissu hata kubeba jukumu zito la kugharamia matibabu yake pamoja na malazi na chakula kwa wategemezi wake aliokwenda nao Ubelgiji ulitoka wapi.

Wazungu wenyewe wabelgiji! ambao juzi tu walikuwa wakiwaita waafrika nyani! Wabelgiji waliokuwa wakiwakata vichwa na mikono waafrika waliochoka kwa kutumikishwa kazi ngumu na madhefuli hao, Wabelgiji wezi wakubwa wa rasilimali za Afrika, ghafla wakawa malaika walinzi wa Lissu!

Waafrika wenzetu hawa walishindwa kabisa  kutumia mbongo zao kujiuliza maswali mepesi kuwa ni kwanini Lissu baada ya kupona hakutaka kurudi nyumbani na badala yake alianza kuzunguka Ulaya na Marekani akiichafua nchi yake, hawakijiuliza nauli ya kuzunguka Ulaya na Marekani aliipata wapi kama aliishiwa hadi pesa ya kula na ya kulipa karo ya watoto wake.

Binadamu wanaojidanganya wana akili walishindwa kuzitumia akili zao kujiuliza ni kwanini Lissu aliamua kwa makusudi tu kukaidi maagizo ya mwajiri wake (Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) lililokuwa likimlipa mshahara mnono na marupurupu kibao ili afukuzwe kazi (Ubunge) na kuendelea na ziara ya kuichafua Tanzania na Watanzania kwa kivuli cha kuombaomba?

Hakuna hata mmoja kati ya waliomchangia aliyejiuliza ni nani aliyelipa gharama za matibabu ya Lissu katika Hospitali ya bei mbaya Ubelgiji ambaye alishindwa kumpa pesa ya kujikimu lakini akaweza kumkatia tiketi ya ndege kuzunguka Ulaya na Marekani kuitukana Tanzania duniani kote.

Waafrika wote waliomchangia walitumia moyo badala ya akili kuyapima maneno yake. Kwa sababu ya udhaifu wa mioyo yao wakadanganyika na ghilba zake wakammiminia mapesa, Waafrika wepesi sana kudanganywa. Lissu akiwa na mapesa yao akaendelea kula kuku Ulaya huku akiwaamisha kuwa iwapo atarejea Tanzania maisha yake yatakuwa hatarini.

Akiwa huko huko Ulaya, Chadema kikafanya uchaguzi kikamchagua kuwa makamu mwenyekiti taifa bila yeye mwenyewe kuwepo. Hakuna mjumbe wa mkutano ule wala mwanachama aliyehoji kuwa mtu ambaye hawezi tena kurudi Tanzania ana umuhimu gani kuliko wengine wote katika kundi hilo hata kupewa wadhfa huo? Lakini pengine ni kwa sababu walijua atarejea kuja kufanya aliyoyafanya wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020 na hata baada ya uchaguzi mkuu.

Lissu, tofauti na alivyoutangazia ulimwengu kuwa hawezi kurejea nchini kwa sababu ya kuhofia usalama wake, siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu alirejea na kupokelewa kwa amani na chereko chereko na wanachama na mashabiki wa kikundi chake.

Safari yake kurejea nchini ilikuwa ya kuja kufanya kazi maalumu aliyoifanya kwa miezi mwili wakati wa kampeni ambayo Watanzania na dunia nzima waliiona.

Aliianza kwa kasi kubwa kwani baada tu ya kutua alimuongoza Mbowe na  viongozi wengine wa Chadema kukiuka utaratibu wa kufika msibani kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu.

 

Alipoelezwa kuwa amekiuka utaratibu kwa makusudi hivyo hataruhusiwa kuingia uwanjani mpaka atakapoufuata akapaza sauti kuwa serikali imeanza kumuonea. Wasiokuwa na akili wakaungana naye kupayuka anaonewa na uongo huo ukasambazwa na wazungu waliomtuma lakini serikali iliupuuza na haina shaka iliupuuza kwa kutumia busara ya kawaida kabisa ya waungwana hawazozani msibani.

Hilo lilipita na walioaminishwa na Lissu kuwa akirejea Tanzania maisha yake yatakuwa hatarani bado wanasubiri mpaka leo yawe hatarini. Wakiwa kwenye kusubiri ndipo alianza kucheza na akili za vijana wachache wa kitanzania ili wamsaidie kuiangamiza Tanzania. Twende taratibu ili tuelewane vizuri.

 

Lissu kwa sababu anajua vijana wengi wa kiafrika wenye akili kama za kwake hawapendi kwao na vya kwao alianza kampeni zake kwa kuhubiri kuwa Watanzania hawana uwezo wa kujitegemea!  Eti! wao ni tegemezi tu kwa wazungu.

Akaenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa mafanikio yaliyofikiwa sasa na Watanzania katika sekta ya madini si lolote wala chochote hivyo akichaguliwa yeye kuwa rais, madini ya Tanzania atayakabidhi kwa wazungu waliomtuma kuja kulichonganisha taifa ili Watanzania wamwage damu.

Haina shaka hata kidogo kuwa kauli hii ys hovyo ya Lissu kuhusu kuyatoa madini yetu kwa wazungu ilibeba makubaliano yake na vinara wa uuzaji madini duniani wakati mataifa yao hayana chembe ya madini.

Wapo Watanzania walioshangilia na walishangilia kwa sababu wana njaa na wana njaa kwa sababu hawataki kufanya kazi. Lissu alicheza na njaa njaa zao, akawadanganya kuwa akiwapa wazungu madini yetu wataishi maisha ya kula bure.

Genge la Watanzania hawa, limesahau kuwa ni juzi tu kabla ya kurekebishwa kwa sheria ya madini, wazungu  waliokusudiwa kupewa madini yetu na Lissu walikuwa wakiwatandika waafrika kama mbwa huko migodini. Wamesahau kuwa dada zetu walikuwa wanafanyishwa mapenzi na mbwa. Tamaa yao ni kula bure. Kwa akili ya kichokonozi, hawa kama walijiandikisha kipiga kura nadhani ndiyo waliompigia kura Lissu.

Wezi, vibaka, majambazi, wazinzi na wazururaji, Lissu amefanikiwa sana kuziteka akili zao. Amewaaminisha wahalifu hawa kuwa amani ni kitu cha hovyo na wao wamemuelewa sana kwa sababu katika machufuko na pasipo na ulinzi na usalama wa raia na mali zao, wahalifu hufaidika kwa kutekeleza vitendo vya kihalifu.

Lissu kwa kutambua akili mbaya za makundi haya alichokifanya ni kuchochea moto katika akili za wezi, vibaka na majambazi wanaokosa vipato haramu kwa sababu serikali inapambana nao kwa kutumia jeshi la Polisi. 

Alifanya hivyo kwa sababu anajua Serikali ya Rais John Pombe Magufuli, imefanikiwa sana katika mapambano dhidi ya wezi, vibaka na majambazi. Taifa sasa liko salama ili kulivuruga lazima kuyachochea makundi ya kihalifu yaanzishe vurugu.

Amani na mshikamo kwa raia wema wa Tanzania ni wa kiwango vya juu sana. Watanzania wachache wahalifu waliofanikiwa kukwepa mikono ya sheria hivyo wapo uraini, wanaishi kwa tabu sana. Na hawa ndiyo aliowalenga Lissu katika harakati zake za kuusaka urais tangu aliporejea nchini.

Hakuna raia mwema wa Tanzania anayeweza kuwa na mawazo ya  kuingia barabarani kuharibu amani ya nchi baada ya mipango ya Lissu kuharamisha utanzania wa watanzania kushindwa, bali wezi, vibaka na majambazi ndiyo wanaoweza kufanya hivyo.

Lissu alitaka yafanyike maandamano ili polisi waje kuwatawanya waandamanaji kisha wao wakaidi, itokee vurugu, wavamie maduka na nyumba za raia wema waibe.

Hilo lingetokea damu ingemwangika na hapo ndipo waliomtuma Lissu wangeshupaza mishipa ya shingo kutaka kuja kutavamia kwa kisingio cha kulinda amani.

Tayari Lissu ameishakimbilia kwa wazungu kwenda kujificha hata kabla hajaulizwa kwanini amepungukiwa adabu hata ile ya kusingiziwa tu. Ili tuwe salama hatuna budi kuwakataza wafuasi wake aliowaacha kwa staili inayorandana na matendo yao maovu.

Historia ni mwalimu mzuri na hutenda haki kwa kila mmoja na kwa kila tukio. Kama ambavyo imekuwa ikitenda haki siku zote, itaendelea kutenda haki kwa kutunza simulizi ya mambo ya hovyo ya Tundu Lissu na genge lake. Tusome historia.

Mwisho.

 


HISTORIA INAPOMTANGULIZA LISSU MBELE  YA KIVULI CHA URAIS WA DHAMBI


NA MWANDISHI WETU

HISTORIA, licha ya kuwa mwalimu mzuri ina tabia ya kujirudia. Matukio mengi, mazuri na mabaya yaliyopata kutokea na yanayotokea sasa yamo katika vitabu vya historia.

Kwa tabia hiyo hiyo ya historia, mwenendo wa uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Oktoba 28, 2020 kwa ujumla; na ule wa wagombea binafsi hususan wale wa kiti cha urais, maneno na matendo yao, bila kujali kama ni mazuri au mabaya yamo katika vitabu vya historia.

Na historia hiyo hiyo ina tabia moja mbaya ya kuadhibu wale wote wasioizingatia. Kwa tabia yake hiyo, pengine kwa  kutambua ghadhabu zake na wepesi wake wa kuadhibu bila huruma wale wote wasiopenda kijifunza kutoka kwayo, imetoa mwanya kwa matendo yake makuu na yenye kuogofya kutunzwa vitabuni na pia kuwa simulizi.

Kwa Watanzania ambao wamo katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa kuchagua rais, wabunge na madiwani, historia kwa tabia yake ilivyo, kwanza imewafunulia 'chapta' inayoelezea kwa kina vita vya mawakala wa mabeberu nchini Libya na imewapa sauti thabiti wasimulizi wa tabia za mabeberu na uchu wao dhidi ya rasilimali ambazo mwenyezi Mungu ameyajalia mataifa ya Afrika na hasa Tanzania ili kupitia historia hiyo, Watanzania wasifanye kosa kama walilofanya Walibya.

Si nia yangu MCHOKONOZI kurejea historia hizo kwa kina lakini hofu yangu dhidi ya ghadhabu ya historia imenisukuma kuwakumbusha Watanzania kuwa kinachoendelea sasa hapa nchini kimo katika vitabu vya historia na tusipoizingatia historia kama itakavyo, haina shaka itatutendea kwa mujibu wa taratibu zake.

Historia inatufundisha kuwa utajiri wa nishati iliyonayo Libya na aina ya kiongozi aliyekuwa akiliongoza taifa hilo kuliifanya imezewe mate sana na mabeberu.

Mabeberu hawakuitamani Libya kwa mema bali waliitamani kwa mabaya, walitamani utajiri wake wa nishati uwe wao na walitamani kiongozi wa taifa hilo, Hayati Muammar Ghadafi awe mzungu lakini kwa sababu hakuwa wao walitamani asiwepo kabisa duniani. Walitamani afe. Waliweka nia ya kumuua. Na walimuua kwa kutumia mikono ya Walibya wenyewe. Hii ni historia.

Wazungu mabeberu walitamani mafuta ya Libya yawe ya kwao, wayauze duniani kote kwa kadri watakavyo ili wawe na pesa za kutosha mifukoni mwao za kunywea kikombe cha kahawa chapa ya Africafe na kutafuna korosho tamu za Mtwara na Lindi kwa kadri ya tamaa zao.

Walitamani watoto na wajukuu zao wakipevuka na kuoana, wapewe nyumba na pesa lukuki za kuanzia maisha tofauti na kwao ambako liwe jua au mvua utu wa mtu hauna thamani bali mtu huthaminiwa kwa mali. Hivyo wako tayari kufanya lolote ili wapate mali isiyokuwa yao.

Mabeberu weupe lakini waovu walitamani Ghadafi awe Rais wao ili ayaongoze mataifa yao kwa mafanikio na kuwapa raha raia wa kizungu kama alivyokuwa akifanya kwa Waafrika wa Libya lakini hilo lilikuwa haliwezekani kwa sababa Ghadafi mwenyewe alikuwa Mwafrika anayejitambua. Alitambua kuwa Mungu hakumuumba kimakosa kuwa mlibya. Alitambua kuwa yeye aliumbwa kwa ajili ya Walibya na Afrika.

Kwa sababu ya uovu wao, watu hao mabeberu weupe waliamini Walibya hawakustahili kuwa na kiongozi bora kama Ghadafi na kwa sababu alikuwa jiwe kweli kweli kwao waliazimia asiwepo duniani. Haya ni kwa mujibu wa historia.

Historia hiyo hiyo inaonyesha kuwa zilipoanza kuzuka vurugu katika mataifa ya kiarabu, mabeberu walijipenyeza kwa nguvu Libya, wakawatumia vibaraka wao na nguvu zao za kijeshi kuuangusha utawala wa Hayati Ghadafi.

Wazungu mabeberu kwa kuwatumia vibaraka wao walipenyeza sumu yao ya uchonganishi, baadhi ya Walibya, kwa ujinga wao wakashawishika na ghilba walizopenyezewa, wakayakataa maisha bora na kuyakaribisha maisha ya kulala mitaani, maisha ya kuwa wakimbizi, maisha ya kukosa huduma za afya, elimu bure, maji, umeme na kila neema waliyokuwa nayo.

Walibya kwa kushawishiwa na vibaraka wa mabeberu wakaikumbatia vita, wakamuua kwanza kiongozi wao Ghadafi aliyewatoa kwenye nchi iliyokuwa jangwa na kuwapeleka kwenye Libya iliyokuwa bora kuliko mataifa ya mabeberu na baada ya hapo wakaanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Leo, Walibya wanapoendelea kuuana, vibaraka wa mabeberu waliowamwangia upupu vichwani mwao kuvuruga akili zao kiasi cha kuzitoa kwenye mawazo ya kijitegemea na kuwa tegemezi, wakimbizi na watumwa. Wao na familia zao wanaishi maisha ya anasa ughaibuni.

Na kwa vibaraka wa mabeberu walioko Libya, kama wapo. Watakuwa wapo kwa ajili ya kutawala kwa niaba ya mabwana zao, mabeberu. Wake na watoto wao hawapo Libya, wanaishi kwa mabeberu. Ni watawala wa dhambi.

Katikati ya mateso hayo ya Walibya, mabeberu wa kizungu wananyonya utajili wa Libya watakavyo. Wanaibomoabomoa Libya kwa silaha nzito nzito kwa kuwatumia Walibya wenyewe.

Walibya na ndugu zao wa Bara la Afrika wanauana katika ardhi ya Libya na viungo vyao; maini, figo pengine hata makanyagio yao vikinyofolewa kwenye miili yao na kuuzwa kwa mafungu kama ziuzwavyo pilipili hoho sokoni. Hii ndiyo ghadhabu ya historia.

'Chapta' katika kitabu cha historia hii ambayo wino wake haujakauka, sasa ipo wazi kwa kila Mtanzania. Ni ama tuisome na kuizingatia ili historia isomeke kuwa Taifa la Tanzania ndilo taifa pekee Barani Afrika lililoepuka ghilba za mabeberu likasonga mbele kuelekea nchi ya maziwa na asali au tuisome na kuipuuza kisha ivimbe kwa hasira na kutuadhibu kwa namna ile ile inavyowaadhibu Walibya.

'Chapta' hii ya historia ya hovyo ya Walibya iliyofunuliwa sasa ili kila Mtanzania aisome na kuamua mwenyewe kuishi kama mtumwa katika nchi yake au kubaki na heshima ya utu wake, bila kuwa ombaomba, maandishi yake yanaumba kivuli cha kiumbe anayefanana na Tundu Lissu, aliyetoka kwa wazungu mabeberu akiwa amevaa pete ya uraia wao, ambaye sasa yupo Tanzania akiwa amefumbata fuko la dhambi tayari  kwa kuiangamiza Tanzania na Watanzania.

Kwa wachokonozi, Lissu kama walivyo binadamu wengine, kwa muonekano wa jinsi alivyofinyangwa na muumba wetu, hana muonekano mbaya ndiyo maana kote anako pita kuwaomba Watanzania wamchague kuwa kiongozi wao mkuu, wanajitokeza kumsikiliza.

Kote anakopita sasa baada ya kutokuwepo nchini kwa muda mrefu nyumbani, wapo wanaokwenda kushangaa muonekane wake, wapo wanaokwenda kuangalia miondoko yake na wapo wanaokwenda kumshangaa anachokisema dhidi ya Taifa la Tanzania na Watanzania wenzake. Haina shaka wapo wanaovutiwa naye na kuamua kuipa kisogo historia.

Nyuma ya historia ya kuangamia kwa Libya kinaonekana kivuli cha Lissu. Maneno na matendo yaliyo ndani ya kivuli hicho vinachora umbo la rais mwovu akiwa amesimama nyuma ya tamaa ya urais wa damu.

Ni kivuli kibaya kukitazama kwa sababu kinaogofya. Kivuli kinachotoa taswira ya rais atakayeligawa Taifa la Tanzania katika makabila - ukanda, kivuli chenye umbo jeusi linalotishia kuzigawa rasilimali za Watanzania kwa mabeberu na katika kivuli hicho hicho, kwa mbali linaonekana umbo la mwanaume shoga akiwa ameachama mdomo wake na kutoa ulimi nje, ishara kwamba ana kiu kali hivyo anasubiri tone la maji baridi kutoka Ziwa Victoria lidondoke kinywani mwake na kumtia nguvu ya kuchomoka kwa kasi nyuma ya kivuli alichopo kuingia mitaani.

Kivuli hiki kilichomtanguliza Lissu katika harakati za kuusaka ukuu wa dola kinamuonyesha katika sura ya mtu mwenye dharau. Sura ya mgombea urais  anayewadharau wapiga kura na kuheshimu mabeberu ambao sifa yao kuu ni kuvuruga amani ya wenyeji, kuwachonganisha na kuwapa silaha ili wauane wenyewe kwa wenyewe wakati wao wakipora mali zao.

Lissu anaonekana mbele ya kivuli cha urais kilichofifia kinachotoa maneno ya dharau na kejeli kwa kiongozi mkuu wa Tanzania anayeheshimika zaidi duniani kwa sasa baada ya kuliwezesha taifa lake kumuangukia Mungu naye akaliinua kwa mkono wake wa kiume dhidi ya gonjwa baya la Corona linalowateketeza walimwengu bila huruma.

Kivuli kilicho nyuma ya Lissu, kinamuonyesha akijaribu kunyanyua mguu apige hatua kuwaelekea Watanzania akiwa amefumbata furushi la dhambi ya kuwahamasisha ndugu zake Watanzania  waingie barabarani kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu ili wamwage damu kabla ya kuchukua mkondo ule ule machafuko ya Libya.

Dunia bado haiamini kuwa mabeberu na kibaraka wao watafanikiwa kuwatumbukiza Watanzania katika vurugu zitakazo liangamiza taifa lao na historia ipo inasubiri kusikia kanusho la kuwakana mabeberu na kibaraka wao kutoka kwenye midomo ya Watanzania wenyewe ifikapo oktoba 28, 2020.

 



Tunapigwa, tujifiche handakini Ufipa



NA CHARLES MULLINDA                                                

VITA inayopiganwa sasa baina ya vikosi vya wanamgambo mamluki wa wazungu dhidi ya wapiganaji shupavu na wenye uzoefu katika medani za vita vya kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imepamba moto.

 

Ni vita ngumu. Inagharimu uhai wa wanajeshi na raia. Wapiganaji wa CCM wanaoongozwa na makomandoo wa kike na kiume waliofuzu kwa viwango vya juu kabisa mafunzo ya vita vya kisiasa vya hovyo na kistaraabu na kwa upande mwingine  wana mgambo mamluki wa wazungu, wanatumia silaha za kisasa na za kale kushambulia na kujihami. Wanatunguana kweli kweli, tena bila huruma.

 

Silaha zinazotumiwa na wana mgambo mamluki wa wazungu ni matusi, kashfa, uzandiki, uongo, upotoshaji na kuwavizia wapiganaji wa CCM kuwanyofoa roho ili wanyamaze milele. Wanajeshi wa CCM wana silaha nyingi sana lakini wamekwishatumia aina mbili tu; moja ni kumwaga sera na kunadi ilani ya chama chao kwa wananchi na pili kuomba kura kwa upole na unyenyekevu.

 

Vita hii kali imeingia katika vitabu vya historia ya siasa za Tanzania kwa sababu tangu kuasisiwa kwa taifa hili haijapata kupiganwa na kwa namna ya pekee imewavutia walimwengu kuifuatilia na hasa mabeberu wanaofadhili vinyamkera wao kwenye uwanja wa mapambano.

 

Leo ni siku ya 10 tangu risasi ya kwanza ilipofyatuliwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya CCM, Rais John Magufuli pale uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuashiria mwanzo wa vita.

 

Tangu kufyatuliwa kwa risasi hiyo, wanajeshi vijana na wenye misuli ya haja wamekuwa wakiwashambulia kwa nguvu wana mgambo mamluki wa mabeberu wa kizungu. Wanawauwa kama kereng'ende.

 

Tayari mwana mgambo mkuu wa jeshi la mamluki ameishajeruhiwa na makomandoo wa CCM. Wapiganaji vijana wa Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli wamemsababishia majeraha ya mwili na akili.

 

Ameanza kusikika akitoa amri zenye matege katika uwanja wa vita. Juzi aliamuru vijana wa msalaba mwekundu walioko mstari wa mbele wakitoa huduma kwa majeruhi wa vita wakusanye vifaa vyao ndani ya dakika 15 watoweke vinginevyo atawashambulia. Amechanganyikiwa.

 

Tathimini ya kuudhi ya kichokonozi ya vita hii inaonyesha kuwa wana mgambo mamluki wa wazungu wamepwaya kwenye uwanja wa vita. Makamanda wao wameanza kwenda nje ya nchi kutafuta misaada.

 

Kundi la wana mgambo linaloongozwa na Mwana mgambo mkuu limechakazwa vibaya na kikosi cha makomandoo wa CCM kinachoongizwa na Amri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

 

Yeye mwenyewe Rais Magufuli  yupo mstari wa mbele, anaongoza vijana wake huku anashambulia. Alianzia Dodoma ambako hakupata upinzani hata kidogo kwa sababu hiyo ni ngome yake kisha aliingia Singida ambako alifyeka wanamgambo mashoga wa wazungu bila huruma. Sasa yupo Geita, kote alikopita ameacha maumivu kwa mamluki.

 

Wana mgambo wa wazungu wapiga propaganda ambao kundi lao lina wanahabari mahili na wasomi nalo limezidiwa mno. Kikosi namba mbili cha makomandoo wa CCM kinachoongozwa na Komandoo mwanamke Mzanzibari ndicho kikosi hatari zaidi dhidi ya wana mgambo mamluki wa wazungu.

 


Kikosi namba mbili cha makomandoo wa CCM kinachoongozwa na Komandoo Samia kimechakaza vinyamkera wa wazungu Mkoa wa Morogoro na baadaye Pwani na kilipoanza kuelekea upande wa kusini kumkabili jasusi muuaji Mwenye roho mbaya, jasusi huyo katoroka, kakimbilia kwa waarabu kuomba msaada.

 

Kundi la wana mgambo wa ardhini ambalo liko mstari mbele katika siasa za majukwaani, wapiganaji wake wengi wameangamizwa na wengine wameachwa na vilema vya kudumu.

 

Wapiganaji mamluki kutoka nje ya nchi waliokodiwa kuja kuongeza nguvu, wengi wao wamekamatwa mateka.

 

Waliosalimika wamebaki na vilema vya maisha. Handaki kubwa la Mtwara sasa sio mahali salama pa kujificha kwa sababu limewekwa katika rada za CCM.

 

Mahali salama ni mtaa wa Ufipa ambako kuna chuo cha kijeshi na mahandaki mengi yaliyochimbwa na wana mgambo kwa ajili ya kujificha nyakati kama hizi wanapopata vipigo vya nguvu.

 

Sasa mbiu ya mgambo imelia. Wana mgambo mamluki wa wazungu popote walipojificha baada ya kusambaratishwa na wapiganaji na makomandoo wa CCM, kimbieni nendeni handaki la Ufipa.

 

Isikieni mbiu inayowapa taarifa za Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya CCM kwamba hivi sasa yupo kijijini Chato amepumzika huku akipata hewa 'fresh' ya Ziwa Victoria kabla yajanyanyuka kuendeleza kipigo. 

 

Ndiyo muda muafaka, jitokezeni nendeni Mtaa wa Ufipa mkajipange upya na kuganga majeraha yenu huku mkizirutubisha upya afya zenu kwa kutibiwa kwenye hospitali zile zile zilizojengwa na Rais Pombe.

 

Wana mgambo mamluki wa wazungu mkiwa mafichoni mtaa wa ufipa ambako mtaishi kwa takriban miaka mitano mkifunzwa taratibu na tamaduni za wapiganaji magaidi kabla ya kurejea uwanja wa mapambano kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, wasanii wa wapiganani wenu watunge nyimbo mpya za kuhamasisha uzalendo na kuinua hamasa ya kila Mtanzania kuyatafuta mabadiliko ya maisha yake yeye mwenyewe badala ya kusubiri kutafutiwa. Labda itasaidia kutibu majeraha makubwa mliyoyapata katika mbongo zenu

 

Nyimbo hizo mziimbe kila asubuhi katika kipindi cha miaka mitano mnapokimbia mchaka mchaka kwa ajili kupasha joto viungo vya miili yenu vilivyojeruhiwa kwa vipigo vya kikatili vya wapiganaji wa CCM.

 

Handakini Mtaa wa Ufipa maofisa wakufunzi wa vita, wajielekeze zaidi kuwafundisha masomo ya sayansi ya siasa badala ya sayansi ya wizi wa kura na wasisahau kutilia mkazo ufundishaji wa somo la athari za kususia shughuli za kitaifa, mikutano ya Bunge, kuandamana andamana na kuheshimu mamlaka zilizoko madarakani.

 

Katika mwendelezo wa mafunzo hayo mapesi na ya awali, wakati wa mijadala jadilini kwa mapana na marefu ni kwanini makamanda wenu wana vimelea vya ushoga na kwanini mwanamgambo mkubwa ni mlevi sana wa konyagi.Jiulize kama hiyo siyo sababu ya kupigwapigwa kama kitenesi na wanapiganaji wa CCM.

 

Kwa ari ya kuyapigania mabadiliko ya kweli ambayo yamehubiriwa na viongozi wenu wana mgambo wa muda mrefu, tumieni pia muda wenu mkiwa handakini kujadili uadilifu wa viongozi wenu. Wawekeni katika mizani ya uadilifu mmoja mmoja mkianza na kamanda Mkuu Mzee wa Konyagi kisha afuate mpenzi wa ushoga.

 

No comments:

Post a Comment