NA MWANDISHI WETU
SERIKALI itawapatia eneo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wasanii
wa sanaa za uchongaji vinyago, uchoraji na sanaa nyingine za ubunifu ili wapate
nafasi kubwa ya kuonyesha kazi zinazoakisi utamaduni wa Mtanzania.
Hayo yameelezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas katika mkutano wake na wadau wa
sanaa za ufundi jijini Dar es Salaam.
Dk. Abbas alisema serikali kupatikana kwa eneo hilo kuwatoa
nafasi kwa Wasanii hao kuuza kazi zao kwa wingi kwa watanzania na raia wa
kigeni kila kunapotea michezo inayozishirikisha timu ndani na nje.
Alisema serikali pia itasimamia kivitendo hoja ya wasanii
hao ya kutaka watanzania wengi watumie kwa wingi sanaa za uchongaji, uchoraji
na nyinginezo za wasanii wa Tanzania.
Katika hatua nyingine, Dk.Abbas alitembelea kituo cha ubinifu
sanaa za muziki, Tanzania House of Talents (THT) alisema serikali haitakiacha
kamwe bali itashiriki kwa karibu kuhakikisha malengo ya kuanzishwa kwake
yanaendelezwa.
Akizungumza na wasanii wa THT katika kituo hicho kilichoasisiwa na marehemu Ruge Mutahaba alisema wizara yake itakiunganisha kituo hicho na Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
No comments:
Post a Comment