NA MWANDISHI WETU
MATUMAINI ya waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari
(2006) Ltd na awali, Habari Corporation Ltd ya kulipwa pensheni zao baada ya
kuondolewa kazini kinyuime cha utaratibu yamezidi kutoweka baada ya kutolewa tangazo
na kusitishwa kwa uchapishaji wa magazeti yanayozalishwa na kampuni hiyo kwa
sababu ya ukata.
Tangazo la kusitishwa kwa uchapishaji wa magazeti yaliyokuwa
yakizalishwa na New Habari (2005) Ltd ya Mtanzania, Rai, Dimba na Bingwa
lilitolewa jana katika mitandao ya kijamii ikimkariri Mhariri Mtendaji, Dennis
Msacky kuwatangazi wafanyakazi wanaodaiwa kuidai kampuni mshahara wa zaidi ya
miezi mitatu, uamuzi huo sambamba za kupunguza wafanyakazi.
Taarifa ya kusitishwa kwa uzalishaji wa magazeti hoyo
ilisomeaka; “Kampuni ya New habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania,
Rai, Bingwa, Dimba imetangaza kusitisha uzalishaji za magazeti yote kutokana na
mwenendo mbaya wa kibiashara.
“Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo, Mhariri
Mtendaji, Dennis Msacky amesema uzalishaji wa magazeti hayo utasitishwa kuanzia
jumatatu ijayo.”
Muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, zaidi ya
watu 150 waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni New Habari waliopunguzwa bila kulipwa
pensheni zao ingawa walikuwa wakikatwa kila mwezi, walianza kuelezea hisia za kuibuliwa
upya kwa machungu ya kupoteza haki zao kwa kueleza kuwa hawana tena uhakika wa
kuzipa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari, Erasto Matasia
alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani kuzungumzia suala hilo alisema yuko
msibani na kwamba aliyeteuliwa na kampuni kuzungumzia usitishwaji huo na
kupunguzwa wafanyakazi kwa niaba ya Hussein Bashe ni Msacky.
“Mimi sipo huko, niko msibani, nakushauri mtafute Dennis
Msacky aliyeteuliwa na kampuni kulizungumzia jambo hilo kwa niaba ya Bashe,”
alisema Matasia.
Jitihada za kumpata Msacky hazikuweza kuzaa matunda baada
ya simu yake ya kiganjani kuwa anaizima kila alipopigiwa na kuita.
Kampuni ya New Habari na kabla ya hapo ikifahamika kwa jina
la Habari Corporation inaandamwa na madeni makubwa ya miaka mingi ya waliokuwa
wafanyakazi wake ambao walikuwa wakikatwa fedha kwa ajili ya pensheni zao
lakini baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni hiyo walikuwa wakizitia kibindoni.
Bashe, ambaye kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge alikuwa
Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 LTD, amepata kukaririwa na baadhi ya vyombo
vya habari akikiri kuchota fedha za kampuni hiyo na kuzitumia katika biashara
zake binafsi na kwamba alikuwa na matarajio ya kuzirejesha baada ya kupata
faida.
Tanzania PANORAMA Blog inaendelea
na ufuatiliaji wa sakata hili
No comments:
Post a Comment