![]() |
Mwenyekiti wa Makampuni ya MeTL, Gulam dewji |
NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Kampuni zilizo chini ya mwamvuli wa Mohamedi
Enterprises Tanzania Limited (MeTL) umesema utatafuta njia ya kumaliza mgogoro
baina yake na wafanyakazi ambao ni raia wa India katika meza ya mazungumzo.
Hayo yameelezwa na mmoja wa maafisa wa kampuni hiyo aliyetumwa
na Mkurugenzi wa MeTL, Gulam Dewji kutoa ufafanuzi kwa Tanzania PANORAMA Blog
kuhusu andishi lililowekwa kwenye mitandao ya kijamii likiwatahadhalisha raia
wa India wote kuepuka kufanya kazi katika kampuni za MeTL.
Andiko hilo mtandaoni linaeleza kuwa Ubalozi wa India umekuwa
ukipokea kwa mfululizo malalamiko ya wafanyaakazi wa Kampuni za MeTL kunyanyaswa
na uongozi pamoja na mwajiri wao kuwafungulia kesi za kughushi mahakamani kiasi
cha kusababisha wanafamilia wa wafanyakazi hao kulazimika kurejea India.
Kwamba Mwenyekiti wa Makampuni ya MeTl, Gulam Dewji na
maafisa waandamizi wamekuwa wakiwafanya vitendo vya unyanyasaji na
udhalilishaji wafanyakazi hao wanapofikisha malalamiko kwao.
Linahitishwa kwamba raia wote wa India wasikubali kuajiriwa
na Kampuni za MeTL kutokana na mwenendo usiofaa wa viongozi wake wa juu.
Alipoulizwa Mwenyekiti Gulam, kuhusu suala hilo kupitia
simu yake ya kiganjani alisema aandikiwe maswali kwa maandishi ili ayajibu na
alipoandikiwa, muda mfupi baadaye mtu mmoja mwenye asili ya kiasia alituma
ujumbe kwa njia ya whatsapp akieleza kuwa ametumwa na Gulam kufikisha ujumbe
kwa Tanzania PANORAMA Blog.
Ujumbe aliuotuma ulisomeka; ‘Bwana Dewji amezungumza na
sisi na ametuhakikishia uwajibikaji wa menejimenti katika kulinda maslahi ya
wafanyakazi. Tumekubaliana kuwa na mazungumzo ya kina, tungependa kutatua jambo
hili kwa njia ya mazungumzo.’
Ujumbe mwingine chini ya huo aliuotuma ulisomeka; ‘leo hii
mmelalamika mazingira ya watu wenu ila tusema ukweli pia mnawanyanyasa sana
watanzania sema tu wanashindwa nani wa kuwasemea pia kutokana na hali za maisha
yao ila mazingira ya ufanyaji kazi siyo.
Jitahidi za Tanzania
PANORAMA Blog kuzungumza na Ubalozi wa India kuhusu suala hili zinaendelea.
No comments:
Post a Comment