NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk. Hassan Abbas emesema watanzania ni watu thabiti ba webte historia ya kutukuka katika mapambano
ya ukombozi wa Bara la Afrika.
Dk Abbas ameyasema hayo jana alipotembelea makao makuu ya
ofisi za Ukombozi wa Bara la Afrika kujionea changamoto zinazoukabili.
Akizungumza katika ofisi hizo, alisema Tanzania ni nchi
yenye watu wenye historia thabiti barani Afrika kutokana na kushiriki kikamilifu
kuzikomboa nchi nyingi barani Afrika.
"Tanzania si tu imetoa mchango mkubwa katika historia
ya Ukombozi wa Afrika bali imegharamika mno kuanzia watu wetu, fedha zetu na
hata kuiweka nchi yetu katika hatari ya kushambuliwa.
“Viongozi wetu walifanya
uthubutu mkubwa na sisi leo sio watu poa, tuko imara kuilinda nchi yetu na sisi
tuliopewa dhamana ya mradi huu lazima tutimize wajibu wetu ili kuitunza
historia hii na kuwajengea vijana wa sasa uzalendo na utamaduni wa kuwa watu wa
kuthubutu kwa ajili ya nchi yao na Afrika," alisema Dk. Abbas.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas
Alisema kutokana na umuhuimu wa ofisi hizo ambazo Umoja wa Afrika (AU) uliamua makao makuu yake yawe Dar es Salaam na serikali imeuweka chini ya usimamizi wa Idara ya Utamaduni katika wizara ya Habari sasa unahamishwa kutoka Idara ya Utamaduni na kuwa moja kwa moja chini ya Ofisi yake.
"Tunataka kwenda kasi
na kwa viwango, wazee wetu walithubutu kufanya mambo makubwa kutufikisha hapa
tulipo, sasa naona mnafanya kazi kubwa lakini mradi huu bado unachangamoto nyingi
ambazo Idara ya Utamaduni pekee haiwezi kuzipeleka kwa kasi, watabaki washauri
wa kitaalamu tu kwangu na kwa mradi huu, lakini kuanzia leo 7, Disemba, 2020,
mratibu wa mradi huu atawajibika na kuripoti moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari," aliagiza Dk. Abbas.
No comments:
Post a Comment