![]() |
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas |
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI iko mbioni kuandaa tamasha kubwa la muziki na sanaa
litakalofahamika kwa jina la moja ya vivutio vikubwa vya utalii vilivyopo hapa
nchini.
Akizungumza wiki hii jijini Dar es Salaam na wadau wa sanaa na
muziki, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.
Hassan Abbas amesema kwa kutambua urithi mkubwa wa sanaa uliopo nchini ukiwemo
muziki, filamu, ngoma na uga mwingine, serikali kwa kushirikiana na wadau,
itaratibu tamasha kubwa la aina yake litakalofanyika baadaye mwaka huu.
Dk. Abbas alisema sekta hiyo inapaswa kuhakikisha inaiburudisha
jamii ya watanzania wachapakazi ipasavyo na kwamba sambamba na kuandaliwa kwa
tamasha hilo, pia serikali kwa kushirikiana na wadau itarejesha tuzo za muziki
na sekta nyingine zilizo chini ya wizara inayoiongoza..
"Moja ya kazi kubwa ya sekta ya sanaa nchini ni kuhakikisha
jamii yetu inayochapa kazi sana kwa sasa inaburudika ipasavyo, sasa naona sanaa
inakuja tu pale panapokuwepo mdhamini au mwandaaji fulani asipokuwepo hakuna
matukio na nchi iko kimya.
"Serikali sasa inakwenda kuchechemsha sekta hii kwa
kuratibu tamasha kubwa sana litakaloanzia Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na
kuendelea kuungana na Tamasha la Kimataifa la Sanaa Bagamoyo.
KAtibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa wizara yake
"Tusisubiri wadhamini, wakija sawa, kama wako likizo basi
mimi nasema sisi wenyewe tunaweza kwa umoja wetu sasa tukutane Uwanja wa Uhuru
Disemba 26 mwaka huu na kisha Desemba 27 twende Bagamoyo.
"Wasanii wakiungana watajaza uwanja. Twende tutateremsha
wasanii wetu wote ambao ni urithi wa sasa na baadaye wa nchi hii halafu tuone
kama watu hawatakuja," amesema Dk. Abbas.
Dk. Abbas yupo katika ziara ya kikazi ya kukutana na wadau
mbalimbali wa sanaa na sekta nyingine zilizo chini ya wizara yake.
No comments:
Post a Comment