![]() |
Mwenyekiti wa Kampuni za MeTL, Gulam Dewji |
NA MWANDISHI WETU
MFANYABIASHARI mwenye
ukwasi wa kutosha ambaye kampuni, viwanda, mashamba na biashara zake zimetoa
ajira kwa Watanzania na raia wa kigeni anatafakari kujibu mapigo dhidi ya Ubalozi
wa India uliyoyataja makampuni yake kuwa siyo sehemu salama kufanya kazi.
Wiki iliyopita, siku moja
baada ta Gulam kumpa maagizo mmoja wa wasaidizi wake kutuma ujumbe kwa Tanzania
PANORAMA Blog wa kusaka suluhu baina ya menejimenti za Kampuni za Mohamedi
Enterprises Tanzania Limited (MeTL) na wafanyakazi wa kigeni wanaodai
kunyanyaswa alisema anajipanga kujibu mapigo.
Gulam alisema amesikitisha
na tamko la ubalozi wa India lililosambazwa mitandaoni kwa sababu linalenga kuwatetea
watu wanaomuibia na kumsumbua.
“Ndiyo nimeliona tamko
kwani nani kasema hajui kuwa ni tamko la Ubalozi wa India, lakini mimi nasema
nakusanya ushahidi halafu nitatoa tangazo kwa vyombo vya habari kwa sababu
ubalozi unatetea wezi, unatetea watu wanaoniibia na kunitesa sana na hata
polisi wanazo taarifa hizi. Sasa ninazungumza na ubalozi halafu nitatoa
statement yangu ambayo mimi nitaitoa kama tangazo,” alisema Gulam.
AWALI Tanzania PANORAMA Blog,
iliripoti kuwa uongozi wa kampuni zilizo chini ya mwamvuli wa Mohamedi
Enterprises Tanzania Limited (MeTL) umesema utatafuta njia ya kumaliza mgogoro
baina yake na wafanyakazi ambao ni raia wa India katika meza ya mazungumzo.
Hayo yameelezwa na mmoja
wa maafisa wa kampuni hiyo aliyetumwa na Mkurugenzi wa MeTL, Gulam Dewji kutoa
ufafanuzi kwa Tanzania PANORAMA Blog kuhusu andishi lililowekwa kwenye mitandao
ya kijamii likiwatahadhalisha raia wa India wote kuepuka kufanya kazi katika Kampuni
za MeTL.
Andiko hilo mtandaoni linaeleza kuwa Ubalozi wa India
umekuwa ukipokea kwa mfululizo malalamiko ya wafanyaakazi wa Kampuni za MeTL
kunyanyaswa na uongozi pamoja na mwajiri wao kuwafungulia kesi za kughushi
mahakamani kiasi cha kusababisha wanafamilia wa wafanyakazi hao kulazimika
kurejea India.
Kwamba Mwenyekiti wa Makampuni ya MeTl, Gulam Dewji na
maafisa waandamizi wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya unyanyasaji na
udhalilishaji wafanyakazi hao wanapofikisha malalamiko kwao.
Linahitimishwa kwamba raia wote wa India wasikubali kuajiriwa na Kampuni za MeTL kutokana na mwenendo usiofaa wa viongozi wake wa juu.
Alipoulizwa Mwenyekiti Gulam, kuhusu suala hilo kupitia simu yake ya kiganjani alisema aandikiwe maswali kwa maandishi ili ayajibu na alipoandikiwa, muda mfupi baadaye mtu mmoja mwenye asili ya kiasia alituma ujumbe kwa njia ya whatsapp akieleza kuwa ametumwa na Gulam kufikisha ujumbe kwa Tanzania PANORAMA Blog.
Ujumbe aliuotuma ulisomeka; ‘Bwana Dewji amezungumza na
sisi na ametuhakikishia uwajibikaji wa menejimenti katika kulinda maslahi ya
wafanyakazi. Tumekubaliana kuwa na mazungumzo ya kina, tungependa kutatua jambo
hili kwa njia ya mazungumzo.’
Ujumbe mwingine chini ya huo aliuotuma ulisomeka; ‘leo hii
mmelalamika mazingira ya watu wenu ila tusema ukweli pia mnawanyanyasa sana Watanzania
sema tu wanashindwa nani wa kuwasemea pia kutokana na hali za maisha yao ila
mazingira ya ufanyaji kazi siyo.
Jitahidi za Tanzania
PANORAMA Blog kuzungumza na Ubalozi wa India kuhusu suala hili zinaendelea.
No comments:
Post a Comment