NA MWANDISHI WETU
JESHI la Polisi limewaruhusu wanafunzi saba wanaosoma
kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya St Mary’s, waliokamatwa wakivuta
dawa za kulevya aina Bangi kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne.
Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog, Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (RPC), Kamishna Msaidizi Ramadhani Kingai amesema,
polisi imewaruhusu wanafunzi hao kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya
sekondari kwa sababu za kiutu na watakapomaliza hatua za kisheria dhidi ya
tuhuma zao zitachukuliwa.
RPC Kingai amesema atatoa taarifa ya hatua
zitakazochukuliwa na polisi Jumatatu, Oktoba 7, 2020a ambapo watakuwa
wamekamilisha uchunguzi ukiwemo wa kutoweka kwa mwanafunzi aliyekuwa akisoma
kidato cha tatu katika shule, Labna Salim Said.
Vijana hao saba ambao majina yao hayajatajwa walikamatwa wakivuta
na wakiwa na misokoto mingi ya bangi ndani ya nyumbani ya Kamishna Msataafu wa
Jeshi la Magereza wakati wa msako wa Labna na baada ya kupekuliwa kwa nyumba
hiyo ilingulika kuwa na shamba la bangi ndani ya ua unaoizunguka.
RPC Kingai alikataa kulitaja jina la Kamishna huyo na
mahali ilipo nyumba yake ambamo walikutwa vijana hao wakiwa na misokoto ya
bangi pamoja na shamba la bangi.
Katika hatua nyingine, RPC Kingai alisema hadi sasa polisi
haijafanikiwa kumpata mwanafunzi Labna lakini juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Uongozi wa Shule ya Sekondari ya St Mary’s haukutoa taarifa
polisi kuhusu kutoweka kwa mwanafunzi huyo na badala yake wazazi ndiyo
walioripoti tukio la mtoto wao kupotea akiwa shuleni.
No comments:
Post a Comment