NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imetoa shilingi bilioni 5.8 kwa shule 151
za Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya kugharamia mpango wa elimu bila
malipo unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarani
mwaka 2015.
Fedha hizi zimenufaisha shule za sekondari 31 na za
msingj 120.
Akizungumza na wananchi wa Shirati kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira Obwere, Kata ya Mkoma, Wilaya ya
Rorya, Mkoa wa Mara, Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema sh. bilioni 3.3 zilitolewa na Serikali ya
Rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya shule za msingi 120.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema fedha hizo zilitolewa
kwa ajili ya ukarabati, masuala ya utawala, michezo, mitihani na posho kwa
maafisa elimu kata na walimu wakuu.
Alisema kwa shule za sekondar 31, Serikali ya Rais
Magufuli ilitoa sh bilioni 2.5 kwa ajili ya fidia ya ada, chakula kwa shule za
bweni na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema serikali kupitia mpango
wa lipa kutokana na matokeo (EP4R) pia ilitoa sh bilioni 1.2 kwa ajili ya
uboreshaji wa miundombinu ya shule ambayo ni pamoja na ukamilishaji wa
miundombinu ya madarasa, vyoo na nyumba za walimu kwa shule za msingi.
Alizitaja baadhi ya shule za msingi zilizonufaika na
mpango huo kuwa ni Mori, Nyanduga, Buchuri, Kondo, Saye, Masonga, Kyaro,
Kitembe, Bubombi, Oliyo B, Dagopa, Nyabi, Ratia, Kotwo, Muchirobi, Manyara,
Ochuna na Nuamaguku.
" Kwa upande wa shule za sekondari zimetumika
sh milioni 777.8 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya shule
ikiwemo maabara, madarasa, mabweni na vyoo kwa shule za Bukama, Mirage,
Ngasaro, Nyamunga, Buturi, Goribe, Nyathorogo, Nyamtinga na Waningo.
Waziri Mkuu Majaliwa yupo Mkoa wa Mara akifanya
kampeni za kumuombea kura mgombea urais wa CCM, Rais John Pombe Magufuli na
aliitumia fursa ya mkutano huo kuwaombea kura mgombea ubunge wa Jumbo la Rorya,
Jafari Chege, mgombea udiwani wa Kata ya Mkoma, Ayoi Mussa Sonde na madiwani
wengine wa wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment