NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imekamilisha ukarabati na upanuzi wa miradi
ya maji katika Wilaya ya Nansio mkoani Mwanza kwa gharama ya sh bilioni 58.
Hayo yameelezwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri
Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
akizungumza na wakazi wa Nansio jana katika uwanja wa Getrude Mongela.
Majaliwa ambaye yuko katika ziara ya kisiasa nchi
nzima ya kumnadi mgombea urais wa CCM, Rais John Pombe Magufuli, amesema kati
ya fedha hizo, sh bilioni 13 zimetolewa kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo sh
bilioni 10.9 za uboreshaji wa huduma ya maji safi mjini Nansio utakaonufaisha
wananchi 108,653.
Amesema sh bilioni 2.1 zimetumika kwa ajili ya
kuboresha huduma ya usafi wa mazingira mjini Nansio.
Ameitaja miradi mingine ya maji iliyokamilishwa na
Serikali ya Rais Magufuli kwa gharama ya sh bilioni 1.3 kuwa ni ukarabati wa
mradi wa maji wa Irugwa, mradi wa maji ya bomba ya Nansore, mradi wa maji
wa Muriti/ Ihebo, upanuzi wa mradi wa maji wa Chabilungo na upanuzi na
ukarabati wa mradi wa maji Kazilankanda.
No comments:
Post a Comment