NA MWANDISHI
WETU
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza masikitiko yake dhidi ya watu
wanaokichafua katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza
na Tanzania PANORAMA, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini
Makene alisema watu wenye nia ovu na chama hicho wamekuwa wakisambaza ujumbe wa
kupotosha katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwatisha au kuibua taharuki
kwa wanachama, wafuasi na mashabiki wa chama.
Alisema
barua iliyosambaa jana mitandaoni inayoonyesha kuandikwa na kusainiwa
naye, Septemba 5, 2020 ni kielelezo cha matendo machafu kinachofanyiwa Chadema
na watu wasiokitakia mema.
"Barua
ya uongo yenye ujinga kama hiyo wanaweza kuamini tu waliyoitengeneza
kujifurahisha kwa mahitaji yao wenyewe kaka," alisema Makene.
Barua
hiyo yenye kichwa cha maneno 'chama cha demokrasia na maendeleo, taarifa kwa
viongozi wote wa kanda ' inaonyesha kusainiwa na Makene na inasomeka;
"Kichwa
cha habari tajwa chahusika. Rejeeni kikao cha tarehe 25.08.2020 ambacho
kilikuwa ni kikao kazi na tathimini ya hali ya fedha kuelekea uchaguzi mkuu
2020.
"Naomba
kuwajulisheni rasmi kuwa tutawezesha kwa asilimia 25% tu na inayosalia tumieni
mfumo wa harambee licha ya ugumu uliopo hasa ukizingatia wafadhili wote wa
ndani kuhofu kutuchangia kwa sababu za kisiasa.
"Pia
tuna taarifa kuwa yapo majimbo ambayo wagombea wetu wameishaingiwa na wasiwasi
wa ushindi na tayari dhamira zao zinatupa mashaka. Hili halikubaliki na tayari
tumeishawatumia timu ya kuchunguza ili kujitathimini kabla ya awamu ya kwanza
ya kampeni kwa mujibu wa vikao vyao vya ndani. Lazima mapambano yaendelee.
No comments:
Post a Comment