Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Bukima, katika mkutano wa kampeni uliyofanyika katika viwanja vya Bukima, wilayani Musoma Vijijin Septemba 20, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imefanikiwa kupunguza utitiri wa kodi
kwenye sekta ya uvuvi katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hayo yameelezwa jana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na
wakazi wa Kata Bukima, Wilaya ya Musoma, mkoani Mara.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa
Shule ya Msingi Majita ambako maelfu ya wananchi walifika kumsikiliza Majaliwa
akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais John Pombe
Magufuli, alisema ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015 -2020
ilielekeza upunguzaji wa kodi kwenye sekta ya uvuvi, agizo ambali limetekelezwa
kikamilifu na Serikali ya Awamu ya Tano.
Majaliwa ambaye aliutumia mkutano huo kuwaombea kura
mgombea ubunge wa Jumbo la Musoma Vijijini, Sospeter Muhongo na madiwani wa
wilaya hiyo, alisema serikali imefanikiwa kupunguza kodi kwenye malighafi na
zana za uvuvi, kuwatambua wavuvi na kuwaweka kwenye vikundi kazi hatua
iliyosaidia kuongeza idadi ya vikundi hivyo kutoka 37 hadi 113.
"Ni kwanini tuliamua kuwaweka kwenye vikundi,
ni kwa sababu inakuwa rahisi kiwafikia, kuwaelimisha na kuwahudumia. Hii
imefanikisha idadi ya samaki wanaovuliwa iongezeke kutoka 415,000 hadi zaidi ya
800,000.
"Kiwango cha uvuaji samaki kimeongezeka kutoka
tani 300 hadi 448,467. Kikubwa ninachowaomba ni kwamba, tumieni vyombo vya
kisasa kuvua samaki ili kutunza mazalio yao," alisema Majaliwa.
No comments:
Post a Comment