NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Mapato (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu
mnada wa pikipiki zilizonadiwa mapema wiki hii baada ya kukaa bandarini muda
mrefu bila kulipiwa ushuru.
Imesema masharti yaliyowekwa katika mnada huo ni ya
kawaida kulingana na aina ya mnada ikizingatiwa kuwa pikipiki hizo hazijalipiwa
ushuru.
Akizungumza leo na TANZANIA PANORAMA Blog,
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema pikipiki hizo
ziliingizwa nchini zikiwa hazijaunganishwa na kukaa bandarini muda mrefu bila
kulipiwa ushuru hivyo TRA ilichukua uamuzi wa kuzipiga mnada.
"Hizo pikipiki ziliingizwa nchini zikiwa
hazijaunganishwa na zipo mara mbili. Kasha la kwanza lina vipande vya pikipiki
25 na la pili lina vipande vya pikipiki 100. Mmiliki wake alishindwa kuzikomboa
hivyo zikaa bandarini muda mrefu zikidaiwa kodi.
" TRA ikatangaza mnada ambao umefungwa jumatano
wiki hii na masharti ni kwamba kwa sababu ziliagizwa kutoka nje ya nchi hivyo
hazijasajiliwa hapa nchini, mnunuzi alipaswa ama kununua ule mzigo
pikipiki zote 25 au ule 100 na siyo moja moja na akishanunua anapaswa
kuzisajili.
"Katika hall ya kawaida mtu binafsi hawezi kuja
kununua pikipiki 25 au 100 kwa ajili ya matumizi binafsi, ni lazima awe
mfanyabiashara ndiyo maana yakawekwa hayo masharti kwamba ni lazima awe na
namba ya mlipa kodi na awe na VAT Kwa sababu baada ya kuzinunua atapaswa kwenda
kuzilipia kodi," alisema Kayombo.
Aidha Kayombo alisema mtu yeyote mwenye wasiwasi
kuhusu mwenendo wa mnada huo au masharti yaliyotumika milango ya ofisi yake ipo
wazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi au kupokea malalamiko.
Awali ilidaiwa na baadhi ya waliotaka kuzinunua
pikipiki hizo kuwa TRA imeweka masharti magumu ya kuzinunua ili kumuwezesha
aliyeziagiza kuweka watu wake wa kuzinunua kwa bei ya mnadani baada ya
kushindwa kuzilipia ushuru.
No comments:
Post a Comment