NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuokoa
asilimia 11 ya vifo vya watu wake vilivyokuwa vikisababishwa na ugonjwa wa
kipindupindu.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Gerard Chami katika mahojiano maalumu ya Tanzania PANORAMA.
Chami alisema ugonjwa wa kipindupindu ulitokomezwa
rasmi hapa nchini Julai mwaka Jana na tangu wakati huo hadi sasa Tanzania
haijapata mtu mwenye mgonjwa huo.
" Taarifa ya kutokomezwa kwa ugonjwa wa
kipindupindu ilishatolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Leonard Subi akizindua
kikao kazi cha kufanya tathimini, maboresho na kuandaa mpango kazi wa miaka
mitano katika kukabiliana na ugonjwa huo hapa nchini.
"Hapa nirejee kukariri kauli ya Dk. Subi kuwa
tangu Julai 2019, Tanzania hatuna Kesi yoyote ya ugonjwa wa kipindupindu.
"Kwa miaka kadhaa halo nyuma tulikuwa na
takriban asikimia 11 ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kipindupindu lakini
kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo
tofauti ikiwemo kuimarishwa kwa miundombinu ya kutolea huduma za afya na
upatikanaji wa dawa na vifaa.
" Pia vifaa tiba na vitendanishi, kaya karibu
zote nchini kuwa na vyoo safi na bora, kuimarishwa kwa usafi wa mazingira na
upatikanaji wa maji safi na salama, kipindupindu kilipungua hadi kufikia
asilimia 1.7 na kwa kipindi cha mwa jana hadi sasa hatuna mgonjwa akiyetolewa
taarifa ya kuwa na maambukizi hayo," alisema Chami.
Alisema kazi inayofanywa sasa na Serikali kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni kuchambua mpango
kazi wa miaka mitano wa udhibiti wa ugonjwa huo, kufanya ufuatiliaji, tathmini
na uperembaji wa afua mbalimbali za Afya hapa na kujua na mpango kazi wa
utekezaji wa kimkakati.
Mwisho

No comments:
Post a Comment