NA MWANDISHI WETU
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kimeshutumiwa kuhusika moja kwa moja na tukio la mauaji ya kinyama ya kijana
Bryan Mollel.
Kwa mujibu wa taarifa ya kulaani mauaji hayo
liyotolewa na Katibu Msaidizi wa Taasisi ya Amani na Maendeleo (TAMA), Mkoa wa
Songwe, Jackson Eliabu inawataja waliohusika na mauaji ya kikatili ya kijana
Mollel kuwa ni viongozi wa Chadema ambao walimpondaponda kwa mawe hadi
alipokufa.
Taarifa ya Eliabu inawataja wagombea udiwani
wa Chadema wa Mkoa wa Songwe kuongoza mauaji hayo kwa sababu ya kulazimisha
wapewe fomu nyingine baada ya kuharibu waliyokuwa nayo.
Sehemu ya taarifa hiyo inasomeka hivi; 'Tumepokea
kwa masikitiko mauaji yaliyofanywa na kuongozwa na wagombea wa udiwani wa
Chadema mkoani Songwe waliyoyafanya hivi karibuni kisa kulazimisha kupewa fomu
nyingine baada ya kuharibu fomu ya awali.
'Taarifa zinaeleza kijana Bryan Mollel aliuawa na
wafuasi na viongozi wa Chadema baada ya juhudi zao za kuhonga hela ili
waruhusiwe kuendelea kugombea kushindikana.'
Taarifa ya Eliabu inaeleza zaidi kuwa mbali ya
kutekeleza mauaji hayo ya kinyama ya Mollel, pia walitaka kumuua kijana
mwingine ambaye aliokolewa na polisi akiwa ameikwishambuliwa na sasa amelazwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
'Mbali na kumpondaponda kwa mawe pia walitaka kumuua
kijana mwingine kabla hajaokolewa na polisi na sasa amelazwa Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya akiwa na hali mbaya.' inasomeka taarifa hiyo.
Taarifa hii ya Eliabu ni mwendelezo ya madai ya muda
mrefu ambayo yamekuwa yakikihusisha Chadema na baadhi ya makada wake na mauaji
wakiwemo viongozi wa juu.
Freeman Mbowe alipata kunyooshewa kidole
akihusishwa na kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Zakayo
Wangwe kilichotokea eneo la Pandambili mkoani Dodoma na alinusurika
kushambuliwa na wananchi wa Tarime alipokwenda kuhudhuria mazishi yake.
Aidha, Chadema kimekuwa kikihusishwa na
matukio mbalimbali ya mauaji katika shughuli zake za kisiasa ikiwemo mikutano
na maandamano

No comments:
Post a Comment