NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga ya Kenya (KCAA) imeondoa
sharti la kuwekwa karantini kwa siku 14 kwa wasafiri wa ndege wanaoingia nchini
humo wanaotokea Tanzania.
Taarifa ya kuondolewa kwa sharti hilo imetolewa
Septemba 16 na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari iliyoeleza kuwa KCAA iliondoa sharti hilo Septemba 15.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali ya Tanzania
nayo imeondoa amri ya kuzuia kampuni za ndege za Kenya kufanya safari zake
nchini Tanzania.
"Kufuatia hatua hiyo, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imeondoa amri ya kuzuia kampuni za ndege za Kenya ikiwemo
Kenya Airways, Fly 540 Limited, Safarilink Aviation na AirKenya Express Limited
kufanya safari zake nchini Tanzania.
" Kwa taarifa hii, sasa kampuni hizo za ndege
za Kenya zimeruhusiwa kurejesha safari zake nchini mara moja na tayari Mamlaka
ya Usafiri wa Anga ya Kenya imejulishwa kuhusu uamuzi huo," ilieleza
taarifa hiyo.
Aidha, katika taarifa yake hiyo, Johari
ilieleza Serikali ya Tanzania itaendelea kuendesha na kusimamia shughuli
za usafiri wa Anga kwa kuzingatia misingi ya kimataifa ya usafiri wa Anga kama
ilivyoainishwa katika Mkataba wa Chicago wa mwaka 1944 na mkataba wa Usafiri wa
Anga baina ya nchi na nchi.
No comments:
Post a Comment