Jengo
la Zahanati ya Kijiji cha Ntope
kilichopo Kata ya Sanza, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida ambalo
ujenzi wake ulianza 2013. Mradi huu unadaiwa kughubikwa na vitendo vya ufisadi
NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya Manyoni mkoani Singida, Rahabu
Jackson amesema anafuatilia madai ya ufisadi katika mradi wa ujenzi wa Zahanati
ya Kijiji cha Ntope iliyopo Kata ya Sanza mkoani Singida.
Akizungumza na TANZANIA PANORAMA BLOG leo, Jackson
amesema taarifa za kuwepo vitendo vya ufisadi katika mradi huo na hasa kufujwa
kwa mamilioni ya fedha za ujenzi zilizotolewa na serikali zilikuwa
hazimjamfikia hivyo ameanza kufuatilia.
"Ni Zahanati, sikuwa na taarifa ndiyo kwanza
nazipata. Nipe muda nakutana na watu sasa hivi nikimalizana nao naanza
kufuatilia madai ya tuhuma hizo," alisema Jackson.
Inadaiwa kuwa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Ntope
ulianza mwaka 2003 lakini mpaka leo haujamalizika.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zimedai
kuwa mwaka 2003 serikali ilitoa shilingi milioni 60 za ujenzi wa zahanati hiyo
ambapo zilitumika sh milioni 20 kujenga msingi na kupandisha matofali machache
kabla ya kudaiwa kuwa sh milioni 40 zimepotea.
Aidha, taarifa nyingine zimedai kuwa fedha hizo sh
milioni 40 zilizokuwa zimesalia kwa ajili ya kukamilimisha ujenzi huo
zilitolewa kwa mkopo zikawekwa kwenye mfuko mwingine wa kijiji lakini
hazijarejeshwa hadi sasa hivyo kukamwisha ujenzi.
Imedaiwa zaidi kuwa licha ya zahanati hiyo
kutokamilika kujengwa, imekuwa ikipatiwa mgawo wa dawa ambazo haijulikani
zimekuwa zikipelekwa kwenye hospitali gani.
No comments:
Post a Comment