Mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya
Chama cha ACT Wazalendo, Said Kubenea amekamatwa na kufikishwa mahakamani
akituhumiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha.
Kubenea amekatwa na polisi Septemba 5, 2020 akiwa
katika gari la abiria lenye namba ya usajili T 645 DKR akitokea mpaka wa
Namanga kuelekea Arusha.
Tayari Kubenea amekwishafikishwa mahakamani mjini
Arusha na kusomewa Mashtaka mawili, la kwanza kuingia nchini kinyume na sheria
ya uhamiaji, sura ya 54 marejeo ya mwaka 2016 na shtaka la pili ni kuingiza
nchini fedha za kigeni bila kutoa tamko kinyume na kanuni za utoaji tamko la
fedha mpakani za mwaka 2016.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga, baada ya kukamatwa na
kupekuliwa alikutwa na Dola za Marekani USD (8000), Shilingi za Kenya
491,700. na shilingi za Tanzania 71,000.
Aidha, Kubenea alikutwa na tiketi ya basi ya la
Super Coach, lenye namba za usajili KCP 4230 ya Septemba 5, 2020 ikionyesha
kuwa siku hiyo alisafiri kutoka Nairobi Kenya hadi mpaka wa Namanga na pia
alikutwa na hati ya makubaliano kati ya Hali Halisi ya Tanzania na Buni Media
Limited ya Kenya.
Vitu vingine alivyokutwa navyo ni risiti ya
malipo ya hoteli iitwayo After 40 Hotels Limited ya jijini Kenya ambayo ilikuwa
imeandikwa jina lake kama mgeni aliyepanga kwenye hoteli hiyo kuanzia Septemba
3 hadi 5, 2020 pamoja na hati yake ya kusafiria.
"Mara baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alieleza
kuwa alifika mkoani Arusha tarehe 2/9/2020 akitokea Dar es Salaam na kufikia
katika hoteli iliyopo Arusha mjini.
" Alieleza zaidi kuwa tarehe 3/9/2020 alikwenda
kulala kwa kaka yake na tarehe 4/9/2020 alikwenda Namanga na kupokea
fedha taslimu tajwa hapo juu kutoka kwa raia wa Kenya.
"Hata hivyo baada ya kupitia ushahidi
uliokusanywa nimebaini kuwa mtuhumiwa Said Ahmed Kubenea hakufikia katika
hoteli aliyoitaja Arusha mjini wala kulala kwa kaka yake kama alivyoeleza.
" Mtuhumiwa tajwa aliingiza nchini fedha za
kigeni bila kutoa tamko rasmi la kisheria kinyume na masharti ya kanuni za
The Anti- Money Laundering ( Cross - Border Declaration of Currency and
Bearer Negotiable Instrument) Regulations, 2016 zikisomwa pamoja na kifungu cha
28b (1) (a) cha sheria ya kuzuia utakatishaji wa fedha haramu Na. 12 ya mwaka
2006." Inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Inasomeka zaidi kuwa baada ya Mkurugenzi wa
Mashtaka, Mganga kujiridhisha na uwepo wa ushahidi wa kutosha dhidi ya
mtuhumiwa pamoja na misingi ya kikatiba inayomuongoza mkurugenzi wa
Mashtaka kama ilivyoainishwa katika ibara ya 59B (4) (a) hadi (c) ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ameidhinisha Mashtaka dhidi
ya Kubenea.
No comments:
Post a Comment