banner

Sunday, November 15, 2020

URAIA WA DIWANI CCM KIVUKONI WAZUA UTATA

 


NA MWANDISHI WETU

Diwani wa Kata ya Kivukoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sharik Choughule anadaiwa kutoa taarifa zisizokuwa sahihi kuhusu uraia wake ili kufanikisha azma yake ya kuwa kiongozi katika chama hicho.

Madai hayo yalianza kusambaa mapema mwezi uliopita lakini jitahada za Tanzania PANORAMA kumfikia kuyazungumzia hazikuweza kufanikiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kutingwa na shughuli nyingi za kisiasa.

Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa kata hiyo aliyefikiwa na Tanzania PANORAMA na kukubali kuzungumza kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa kwa madai kuwa hataki aonekane ana nia mbaya dhidi ya mbio za kusaka uongozi wa kisiasa za Choughule, alisema awali kulikuwa na utata huo lakini ulitatuliwa.

Taarifa zilizokusanywa Tanzania PANORAMA zimeonyesha kuwa Choughule aliingia nchini kwa kutumia hati ya kusafiria ya India akiwa ameambata na ndugu yake wa kiume, ambao walikuja kumtembelea mjomba wao anayefanya biashara jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi umeonyesha kuwa Choughule na ndugu yake walikuja nchini kuonana na mjomba wao aliyekuwa ametwaa mali za baba yao baada ya kufariki dunia.

Washirika wa karibu wa Choughule wamekaririwa kuwa vijana hao wawili walishindwa kuafikiana na mjomba wao ndipo walipogoma kuondoka nchini kurejea India walikokuwa wakiishi na mama yao.

Kwamba ili kuzika mzozo baina yao, mjomba wao aliwaingiza katika moja ya kampuni zake kufanya kazi huku akiwataka wawe na subira ya kutatua utata wa umiliki wa mali hizo.

Imeelezwa kuwa mjomba (jina limehifadhiwa kwa sababu hajapatikana kuzungumza) alitoa taarifa ofisi za uhamiaji kuhusu uwepo wa vijana hao waliokuwa wakiishi nchini na kufanya kazi kinyume cha sheria na walikamatwa na taratibu za kuwarudisha India zilianza kufanyika.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa vijana hao walilia na kupiga magoti mbele ya mjomba wao wakimuomba azungumze na maofisa wa Uhamiaji ili wasirejeshwe India kwa sababu walikuwa wakiishi maisha ya shida na mama yao baada ya baba yao kufariki na kwamba mjomba wao alikuwa hawatumii fedha kama alivyokuwa akifanya baba yao licha ya kujimilikisha mali zote.

Inadaiwa mjomba wao aliwapa sharti la kutomuuliza tena kuhusu mali alizotwaa kwa marehemu kama wanataka kiendelea kuwepo Tanzania, amri ambayo waliiafiki na yalifanyika mazungumzo wakaachiwa.

Afisa mmoja wa CCM wa Kata ya Kivukoni ambaye jina lake limehifadhiwa ameeleza kuwa ni kweli vijana hao waliingia nchini wakitokea India na kufikia kwa mjomba wao kabla ya kukamatwa na maofisa uhamiaji ambao waliwapakia kwenye ndege na kuwarudisha India ambako walikataliwa kuingia na kurudishwa hapa nchini.

"Ni kweli Choughule alikuja nchini akiwa na mwenzake. Walikuja kwa mjomba wao lakini baadaye kulitoka mtafaruku wakakamatwa na uhamiaji wakapandishwa ndege wakarejeshwa India ambako hawakupokelewa walirudishiwa uwanja wa ndege, wakarejea Tanzania.

"Hakukuwa na namna ikabidi wapokelewe hapa nchini wakarudi tena kuishi na mjomba wao ndipo zikaanza kufanyika taratibu za uraia na uhamiaji iliwasafisha kwa kuwapa uraia wakawa huru kujihusisha na shughuli za kisiasa na mpaka sasa Choughule anaendelea na siasa," alisema.

Choughule amekuwa akikwepa kulizungumzia suala hilo kwa zaidi ya wiki tatu sasa kwani licha ya Tanzania PANORAMA kufika ofisi za CCM Kata ya Kivukoni ambako hakupatikani na kisha kutafutwa kwa simu yake ya kiganjani na kuomba apewe muda kabla ya kuzungumza, hajatekeleza ahadi yake hiyo wala kujibu maswali aliyotumiwa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphery Polepole ambaye alitafutwa kwa simu yake ya kiganjani kuzungumzia suala hilo, simu yake imekuwa ikiita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe wa maandishi kwenye simu yake hakuujibu.

Kwa mujibu wa taratibu za Idara ya Uhamiaji, raia wa kigeni anaweza kupewa uraia kabla ya kuwa na sifa za kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa isipokuwa urais wa Tanzania akiishi nchini kuanzia miaka nane na kufuata taratibu za kuomba uraia ikiwemo muda wote wa kuishi nchini kuwa na kibali.

Tanzania PANORAMA limeperuzi sifa zinazotakiwa kwa wanachama wa CCM kugombea uongozi wa kisiasa ambapo ya kwanza inasomeka awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Friday, November 13, 2020

WAZAZI WA MWANAFUNZI ALIYEPOTEA ST. MARY'S WADAI KUPEWA SIRI NYETI NA MKUU WA SHULE

 


NA MWANDISHI WETU

WAZAZI wa mwanafunzi aliyepotea tangu Oktoba 4, 2020 Labna Salim Said wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Bweni Wasichana ya St Mary's iliyopo Mbezi Makonde, Dar es Salaam wamesema Mkuu wa Shule hiyo Reca Ntipoo, aliwafichulia siri nyeti inayowawezesha wanafunzi kutoroka usiku kwenda kufanya ukahaba.

Mwanafunzi Labna anadaiwa kutoroka shuleni usiku akiwa na wenzake na kwenda kwa wanaume lakini tofauti na wenzake ambao walirejea shuleni kabla ya kupambazuka, yeye hakurejea na haifahamiki yupo wapi hadi sasa.

Taarifa za kutoweka kwake ziliripotiwa kwa mara yake na matroni anayetajwa kwa jina Sarah Murra lakini katika hatua ya kushangaza, uongozi wa shule ya St Mary’s haujapata kuripoti tukio hilo polisi na sasa wazazi wa mwanafunzi huyo wanahofia kuwa ameuawa.

"Mkuu wa Shule alituambia kuwa ukuta wa shule hiyo ni mfupi unaowawezesha wanafunzi kuruka kwa urahisi na alisema shule ina walinzi wachache ambao hawatoshelezi kulinda eneo lote la shule ndiyo maana ni rahisi kwa wanafunzi kutoroka usiku," alisema Maduhu.

Mkuu wa Shule, Ntipoo kwa siku kadhaa sasa imekuwa ikiita bila kupokewa.

 

MAKACHERO WANAOCHUNGUZA KASHFA YA UNYANYASAJI KINGONO WALALAMIKIWA

 






NA MWANDISHI WETU

MLALAMIKA katika shauri la madai ya kunyanyaswa kingono (jina limehifadhiwa) amewaelekezea lawama makachero wa polisi wa Kituo cha Chang'ombe wanaochunguza shauri lake kuwa wameuweka pembeni ushahidi muhimu wa madai yake.

Amesema makachero hao ambao wameizuia simu yake ya mkononi kwa uchunguzi hawakuchukua simu ya anayemtuhumu ambayo ina ushahidi muhimu wa kuthibitisha madai yake.

Mlalamikaji huyo anamtuhumu Dreva wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB), anayefahamika kwa jina la Idi Mzee kumnyanyasa kingono.

Kamanda wa Upelelezi (RCO) wa Kituo cha Polisi Chang'ombe, Jumanne Mkwama amekwishathibitisha kuwepo kwa shauri hilo kwa kueleza kuwa simu za mlalamikaji na mlalamikiwa zimepelekwa kwa watalaamu kuchunguzwa.

Kamanda Mkwama aliieleza Tanzania PANORAMA kuwa kinachochunguzwa na makachero wake ni nani kati ya wawali hao aliyevunja mkataba wa kuachana lakini madai mengine yataamriwa mahakamani.

"Sina imani na wapelelezi wa shauri langu. Mimi na Idi katika mambo yetu ya hovyo tulikuwa tunawasiliana kwa WhatsApp. Na hiyo laini yake yenye WhatsApp ndiyo alikuwa akinitumi hela nyingi.

"Ajabu walichukua simu yangu ya WhatsApp lakini ya kwake wakamuachia wakachukua ya kitochi ambayo haina ushahidi wa maana. Niliwaambia simu yake ya WhatsApp ndiyo ina mambo yetu yote wakasema hiyo hawaitaki wanataka kile kitochi.  Nina wasiwasi wanataka kuficha kitu au kumlinda," alisema.

 


Monday, November 9, 2020

WANASHERIA WACHAMBUA KASHFA INAYOMUANDAMA DREVA WA SSB

 


NA CHARLES MULLINDA

KITENDO cha kumshawishi mtu kufanya mapenzi na mnyama au watu watu wawili kufanya mapenzi mbele ya mtu mwingine au mbele ya kadamnasi ya watu ni kosa jinai.

Hayo yameelezwa na wanasheria waliozungumza na Tanzania PANORAMA kuhusu sakata linalomuandama Idi Mzee ambaye ni dreva wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) anayelalamikiwa na mpenzi wake, jina limehifadhiwa kuwa amekuwa akimfanyisha mapenzi na mbwa, kumfanyisha mapenzi na wanawake wenzake, kumfanyisha mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja huku yeye akiwaangalia kabla ya kushiriki naye tendo hilo na pia kumfanyisha mapenzi kinyime cha maumbile.

Hata hivyo, wanasheria hao waliozungumza kwa sharti la majina yao kuhifadhiwa kwa kile walichodai kuwa madai hayo yanatia kinyaa wamesema mwanasheria anayedaiwa kusimamia mkataba wa wapenzi hao kuachana kwa sharti la kulipana pesa hana hatia na alichokifanya hamkimfungi kisheria.

“Mwanasheria anayedaiwa kusimamia mkataba wa wapenzi hao kuachana, na sitaki kumtaja jina mimi hata kama ametajwa kwa sababu ya jambo lenyenye hili lilivyo hana kosa lolote. Hata kama alijua matendo machafu ya watu hao hana kosa. Mwanasheria ni kama karani tu.

“Na huo mkataba aliowasainisha na kulipana fedha kama inavyodaiwa, pamoja na kwamba aliuandaa yeye kama inavyodaiwa lakini hautambuki kisheria.

“Lakini sasa, kitendo cha kufanya mapenzi na mbwa ni kosa kisheria na mtu yoyote anayemshawishi mtu mwingine kufanya mapenzi na mbwa anakuwa ametenda kosa la jinai. Hilo haliko katika makosa ya madai,” alisema mmoja  wa wanasheria waliozungumza na Tanzania PANAROMA.

Mwanasheria mwingine aliyezungumzia hilo alisema binadamu kufanya mapenzi na wanyama hairuhusiwi kisheria.

“Binadamu kufanya mapenzi na mnyama hairuhusiwi kisheria na au kufanya mapenzi kinyume cha maumbile au kufanya mapenzi na mtu zaidi ya mmoja.

“Sisi kama taifa la watu wastaarabu tena wenye utamaduni mzuri kabisa tunapaswa kuyapiga vita kwa nguvu zetu zote mambo ya aina hii pasipo kuagaliana usoni.

“Mwaka 2008, huko mkoani Mwanza, Hakimu  Gadiel Mariki aliwahukumu watu watatu kwenda jela miaka 20 kwa makosa ya kushawishi na kufanya mapenzi na mbwa. Hawa walikuwa wafanyakazi wa kampuni moja inayojihusisha na uchumbaji madini hapa nchini hivyo ni lazima watu waelewe kufanya mapenzi na wanyama au mbele ya mtu mwingine ni makosa makubwa kisheria,” alisema.

WAZAZI WA MWANAFUNZI ALIYEPOTEA ST. MARY’S WAHOFIA KAUAWA

 

Labna Salim Said, mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Bweni Wasichana ya St. Mary's iliyopo Mbezi Makonde ambaye amepotea kwa zaidi  ya mwezi mmoja sasa 

NA CHARLES  MULLINDA

WAZAZI wa mwanafunzi msichana, Labna Salim Said wa Shule ya Sekondari ya Bweni Wasichana ya St. Mary’s ambaye alitoroka shuleni usiku na kutokomea kusikojulikana wameeleza kuwa wanahofia mtoto wao kauawa.

Zephania Maduhu ambaye ni mjomba wa mwanafunzi huyo anayesoma kidato cha tatu na pia mlezi wake, ameieleza Tanzania PANORAMA kuwa mtoto wake alipotea tangu Oktoba 4, 2020 akiwa chini ya uangalizi wa shule na hadi sasa hajapatikana.

Alisema taarifa za kupotea kwa mwanafunzi huyo zilitolewa Oktoba 8, 2020 na matron wake aliyemtaja kwa jina la Sarah Murra aliyempigia simu mama mzazi wa mwanafunzi huyo akiulizia kama ameishafika nyumbani.

“Huyo mtoto ninamlea mimi, ninamlipia ada ya shule mimi, ni mtoto wa dada yangu, anasoma St. Mary’s Mbezi Makonde. Oktoba 8, mwaka huu, matron wake anaitwa Sarah Murra, alimpigia simu mama yake, yaani dada yangu akimuuliza kama Labna kafika nyumbani.

“Dada yangu ambaye wakati huo alikuwa mkoani Shinyanga akashangaa akamuuliza amefikaje nyumbani wakati yupo shule au shule zimefungwa ghafla tena? Yule matron akamjibu ametoroka shuleni tangu Oktoba 4, 2020 hivyo alikuwa anataka kujua kama yupo nyumbani, dada akamwambia yeye yupo mkoani Shinyanga na anajua mtoto wake yupo shule.

“Aliporudi kutoka safari Shinyanga akakuta mtoto hajapatikana na shule haijatoa taarifa polisi yaani hata wasiwasi hawana. Ikabidi yeye aende kutoa ripoti Kituo cha Polisi cha Stakishari, waliniponipa taarifa mimi nikafunga safari mpaka shuleni.

“Pale shuleni nikamkuta mkuu wa shule anaitwa Reca Ntipoo, akanijibu mtoto alitoroka shule usiku hajarudi na hawajui alipokwenda. Nikauliza kama wamefanya jitihada zozote za kumtafuta na kama wameisha ripoti polisi akasema hilo ni jukumu letu wazazi.

“Sasa hapo nikakasirika nikamuuliza mtoto tumemkabidhi shule na ada tumelipa kumbe katoroka zaidi ya mwezi hata taarifa polisi hawajatoa, hapo akajibu labda tukamtafuta kwenye vijiwe vyao vya usiku wakitoroka huwa wanakwenda huko ambako wanafunzi wenzake wanavijua, akamuuita mwanafunzi mmoja kweli akatuelekeza huko wanakokwenda usiku.

“Nilikuwa na rafiki yangu alinisindikiza tukaenda kumtafuta huko hatukumpata, hatukuwa na jinsi ikatubidi sisi tukatoe taarifa nyingine kituo cha Polisi Goba na polisi tulipowaelezea nao walishangaa  kweli kweli.

“Sasa RB tunayo ni STK/RB/10714/2020 na mpelelezi wa shauri hilo ni Afande Gwake Mwakapande. Sidhani kama yupo hai sisi tunaamini ameishakufa lakini uongozi wa shule hii ndiyo umetuulia mtoto wetu. Polisi wanajua sasa sijui kama wameishawauliza au bado,” alisema Maduhu.

Alipoulizwakwa simu yake ya kiganjani, Afande Mwakapande kama analifahamu suala hilo alisema ni kweli faili la uchunguzi la kupotea kwa mtoto huyo analishughulikia yeye lakini yuko kwa kinyozi ananyoa nywele hivyo akimaliza atapiga simu  kuelezea alipofikia katika upelelezi wake, jambo ambalo hakulitekeleza.

Mwisho.