NA MWANDISHI WETU
MLALAMIKA
katika shauri la madai ya kunyanyaswa kingono (jina limehifadhiwa)
amewaelekezea lawama makachero wa polisi wa Kituo cha Chang'ombe wanaochunguza
shauri lake kuwa wameuweka pembeni ushahidi muhimu wa madai yake.
Amesema
makachero hao ambao wameizuia simu yake ya mkononi kwa uchunguzi hawakuchukua
simu ya anayemtuhumu ambayo ina ushahidi muhimu wa kuthibitisha madai yake.
Mlalamikaji
huyo anamtuhumu Dreva wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB), anayefahamika
kwa jina la Idi Mzee kumnyanyasa kingono.
Kamanda wa Upelelezi
(RCO) wa Kituo cha Polisi Chang'ombe, Jumanne Mkwama amekwishathibitisha kuwepo
kwa shauri hilo kwa kueleza kuwa simu za mlalamikaji na mlalamikiwa zimepelekwa
kwa watalaamu kuchunguzwa.
Kamanda Mkwama
aliieleza Tanzania PANORAMA kuwa kinachochunguzwa na makachero wake ni nani
kati ya wawali hao aliyevunja mkataba wa kuachana lakini madai mengine
yataamriwa mahakamani.
"Sina imani na wapelelezi wa shauri langu. Mimi na
Idi katika mambo yetu ya hovyo tulikuwa tunawasiliana kwa WhatsApp. Na hiyo
laini yake yenye WhatsApp ndiyo alikuwa akinitumi hela nyingi.
"Ajabu walichukua simu yangu ya WhatsApp lakini ya
kwake wakamuachia wakachukua ya kitochi ambayo haina ushahidi wa maana.
Niliwaambia simu yake ya WhatsApp ndiyo ina mambo yetu yote wakasema hiyo
hawaitaki wanataka kile kitochi. Nina
wasiwasi wanataka kuficha kitu au kumlinda," alisema.
No comments:
Post a Comment