NA MWANDISHI WETU
ALIYEKUWA Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (RPC), Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
Edward Bukombe, amehamishwa kituo chake cha kazi na kupelekwa makao makuu.
Taarifa
zilizoifikia Tanzania PANORAMA Blog kutoka vyanzo vyake vya habari zimeeleza
kuwa Kamanda Bukombe sasa anakwenda kuongoza kitengo cha picha na matukio na
kwamba uhamisho huo ni wa kawaida.
Kwa mujibu wa
taarifa hizo, nafasi ya Kamanda Bukombe imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa
Polisi, Ramadhani Kingai ambaye katika mahojiano yake leo na Tanzania PANORAMA Blog
amethibitisha kurithi wadhfa huo akitokea mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment