NA MWANDISHI MAALUM
KATIKA kunogesha zaidi msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka
na mwaka mpya, Kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza ofa kabambe kwa
wateja wapya wa DStv yenye lengo la kuhakikisha Watanzania wengi wanapata
huduma hiyo ili waweze kufurahia burudani, elimu na habari wao na familia zao
msimu huu wa sikukuu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya DStv ya msimu
wa sikukuu iliyopewa jina la ‘Vibe la sikukuu na DStv kama DStv’, Mkuu wa
Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema kama ilivyo ada kwa
DStv, kila unapofika msimu wa sikukuu hutoa ofa maalum kwa wateja wake ili
kuwapa uhakika wa kupata huduma za DStv kipindi cha sikukuu na watu wengi
wakiwemo watoto huwa likizo hivyo kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa burudani
nyumbani.
Akifafanua, Shelukindo amesema kampeni ya msimu wa sikukuu DStv
hutoa ofa maalum kwa wateja wake.
“Kwa wale ambao bado hawajajiunga na DStv, huu ndio wakati
muafaka kwani kuna ofa maalum ya kujiunga ambapo mteja ataunganishwa na DStv
kwa Sh,79,000 tu na zawadi ya kifurushi cha Family mwezi mmoja bila malipo”
alisema Shelukindo.
Alisema ofa hii inawapa uhakika wateja wapya kufurahia
maudhui motomoto ndani ya DStv na itadumu hadi mwisho wa mwezi Desemba 2020.
Mkuu wa Mauzo wa MultiChoice Tanzania, Salum Salum akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msimu wa sikukuu ambapo DStv imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake
Akifafanua zaidi kuhusu ofa hiyo alisema inapatikana nchi
nzima kwa mawakala wa DStv hivyo mteja atapata ofa hii na huduma ya kufungiwa
DStv popote alipo kwa urahisi na haraka.
“Tunafahamu kuwa kipindi hiki cha sikukuu watu wengi
husafiri kuungana na familia zao maeneo mbalimbali mijini na vijijini na kwa
kulitambua hili tumejipanga kuhakikisha huduma zetu zinapatikana kirahisi kila
mahali”
Amewashauri wateja wote ambao wanahitaji huduma za DStv,
mbali na kwenda kwenye vituo au mawakala wa DStv, wanaweza pia kupata huduma
hiyo kwa kupiga simu 0659070707 au kwa kutembelea kurasa za DStv Tanzania za
mitandao ya kijamii Instagram @dstvtanzania, Twitter @DStv_Tz na Facebook
@DStv(tz) ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali za DStv kama vile kuunganishwa,
kulipia vifurushi, kubadili kifurushi na huduma nyinginezo.
Kwa wateja wa DStv, Salum amesema wataendelea kupata
maudhui kemkem kuanzia michezo, burudani, vipindi vya elimu, chaneli za watoto,
sinema na tamthilia za ndani na nje bila kusahau chaneli za habari
zitakazowahakikishia taarifa mbalimbali kutoka pande zote za dunia.
Kwa wale wanaosafiri, amewakumbusha kupakua App ya DStv Now
inayowawezesha kuendelea kufurahia huduma za DStv kwenye vifaa mbalimbali kama
simu janja bila gharama yaziada.
“Kwa wale wanaosafiri na wangehitaji kuendelea kuburudika
na DStv, ni vyema wakatumua huduma yetu ya DStv Now kwa kupakua app yetu na
hivyo kuweza kutumia akaunti zao katika vifaa zaidi ya vine popote walipo
nchini bila kulazimika kulipia malipo yoyote ya ziada” alisisitiza Salum
Waigizaji maarufu katika tamthilia ya Karma Ford (kulia) na Misa (Katikati) wakiwa pamoja na maafisa wa DStv Tanzania – Mkuu wa Masoko Ronald Shelukindo (wa pili kulia), Mkuu wa Mauzo Salum Salum (wa pili kushoto) na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Grace Mgaya (kushoto) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msimu wa sikukuu
No comments:
Post a Comment