NA CHARLES MULLINDA
MKATABA wa kuvunja uhusiano binafsi wa wapenzi
wawili unaodaiwa kughubikwa na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono
uliandaliwa na kusainiwa mbele ya mwanasheria wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa
(BSS)
Uchunguzi wa Tanzania PANORAMA umebaini kuwa mkataba
huo uliandaliwa na kusainiwa ili kuvunja uhusiano wa kimapenzi baina ya Idi
Mzee ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya BSS na mwanamke mpenzi wake ambaye jina
lake limehifadhiwa.
Imebainika kuwa mwanamke huyo alikwenda kwa
mwanasheria wa BSS kumlalamikia Idi kwa kutomlipa ujira wa kazi aliyokuwa
amempa ya kufanya tendo la ndoa na wanaume tofauti tofauti huku yeye akitazama
kabla ya kushiriki naye pia.
Kwamba mwanamke huyo alidai kuwa alikuwa akichukua
wanaume tofauti kwenda kushiriki nao tendo la ndoa mbele ya Idi kwa makubaliano
waliyokuwa wamefikia na Idi kuwa watakuwa wakiwalipa lakini katika hatua ya
kushangaza Idi alianza kuchelewesha malipo hayo.
“Mwanasheria huyo alimuita Idi na kumuuliza kama
anamfahamu huyo mwanamke akakubali, akamuuliza kama madai ya mwanamke huyo kuwa
alimpa maelekezo ya kutafuta wanaume na kuwapeleka kwake kushiriki nao tendo la
ndoa kabla ya kushiriki naye pia akakubali lakini alisema anataka waachane.
“Ndiyo mwanasheria akaandaa mkataba wa kuwaachanisha
kwa makubaliano kuwa Idi alimlipe huyo mwanamke shilingi milioni mbili kisha
kila mtu aendelee na maisha yake, ajabu wiki mbili baada ya kusainiwa kwa
mkataba huo, Idi alimpigia simu huyo mwanamke akimuomba amtumie picha zake
chafu ili aweze kufanya jambo lake kwa ahadi kuwa atamlipa lakini alipotumiwa
hakumlipa ndiyo mgogoro ukaanza upya.
“Tatizo hapo ni pesa, yule Idi anatumia pesa nyingi
anazodai kuzitoa kwa bosi wake ambaye huwa anamfanyia kazi maalumu na hawa dada
zetu wana njaa sana ndiyo maana wanaharibu kabisa maadili yetu, wanahatarisha
maisha yao na ya wengine na wanachafua majina ya kampuni zao na mabosi wao.
“Na ajabu hizi sheria nazo zinaruhusu mambo mabaya
mno kwa sababu mwanasheria kusimamia makubaliano ya kisheria kwa mtu anayedai
mpaka aliyefanyishwa kitendo hicho na mbwa nadhani si sawa,” alisema mtoa
taarifa wa Tanzania PANORAMA.
Wakati haya yakibainika, tayari Jeshi la Polisi
limeeleza kuwa linasubiri uchunguzi wa kitaalamu wa simu za mkononi za Idi Mzee
na mpenzi wake anayemtuhumu kumnyanyasa kingoni pamoja na kumfanyisha tendo la
ndoa na mbwa ili hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa.
Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa
Mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, Jumanne Mkwama ameiambia Tanzania PANORAMA kuwa kinachochunguzwa na
polisi ni nani kati ya wawili hao aliyevunja mkataba wa kuvunja uhusiano wa
kimapenzi ambao ulisainiwa baada ya kutoelewana kwao.
Alisema mambo mengine yanayolalamikiwa na mwanamke
huyo dhidi ya Idi, yatashughulikiwa na mahakama.

No comments:
Post a Comment