banner

Friday, November 13, 2020

WAZAZI WA MWANAFUNZI ALIYEPOTEA ST. MARY'S WADAI KUPEWA SIRI NYETI NA MKUU WA SHULE

 


NA MWANDISHI WETU

WAZAZI wa mwanafunzi aliyepotea tangu Oktoba 4, 2020 Labna Salim Said wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Bweni Wasichana ya St Mary's iliyopo Mbezi Makonde, Dar es Salaam wamesema Mkuu wa Shule hiyo Reca Ntipoo, aliwafichulia siri nyeti inayowawezesha wanafunzi kutoroka usiku kwenda kufanya ukahaba.

Mwanafunzi Labna anadaiwa kutoroka shuleni usiku akiwa na wenzake na kwenda kwa wanaume lakini tofauti na wenzake ambao walirejea shuleni kabla ya kupambazuka, yeye hakurejea na haifahamiki yupo wapi hadi sasa.

Taarifa za kutoweka kwake ziliripotiwa kwa mara yake na matroni anayetajwa kwa jina Sarah Murra lakini katika hatua ya kushangaza, uongozi wa shule ya St Mary’s haujapata kuripoti tukio hilo polisi na sasa wazazi wa mwanafunzi huyo wanahofia kuwa ameuawa.

"Mkuu wa Shule alituambia kuwa ukuta wa shule hiyo ni mfupi unaowawezesha wanafunzi kuruka kwa urahisi na alisema shule ina walinzi wachache ambao hawatoshelezi kulinda eneo lote la shule ndiyo maana ni rahisi kwa wanafunzi kutoroka usiku," alisema Maduhu.

Mkuu wa Shule, Ntipoo kwa siku kadhaa sasa imekuwa ikiita bila kupokewa.

 

No comments:

Post a Comment