NA MWANDISHI WETU
JESHI la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wataombwa
kumsaka mwanafunzi aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Bweni ya St. Mary’s
iliyoko Mbezi Makonde, Labna Said Salim ambaye ametoweka tangu Oktoba 4, 2020.
Taarifa iliyotolewa
na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kinondoni, Joseph Kapere kwa Tanzania
PANORAMA Blog leo, imeeleza kuwa taasisi hizo zitaombwa kusaidia kumsaka
mwanafunzi huyo popote alipo baada ya jitihada za Jeshi la Polisi kumsaka
kushindwa kuzaa matunda.
Kapere
ambaye alikuwa akizungumzia mwenendo wa uchunguzi wa timu ya maafisa wanne wa serikali
iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo kuchunguza mazingira
ya kutoweka kwa mwanafunzi huyo na kumsaka mahali alipo, ameeleza kuwa tume
hiyo imekwishamkamata kijana anayedaiwa kuishi na mwanafunzi huyo baada ya
kutoroka shuleni na sasa inasubiri wanafunzi wa kidato cha nne wamalize
mitihani ya taifa ili iweze kuchukua hatua zaidi.
Timu
hiyo inayomsaka mwanafunzi huyo inaundwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya
Kinondoni, Afisa Usdalama wa Wilaya ya Kinondoni, Afisa Elimu Sekondari wa
Wilaya ya Kinondoni na Mdhibiti Ubora wa Elimu Kanda.
“Uchunguzi
wetu unaendelea lakini hatufanikiwa kumpata huyo mtoto. Tiumekwishamkamata na
kumuhoji kijana ambaye inadaiwa kuwa yule mtoto alitorokea kwake, anakiri
kwamba ni kweli alikwenda chumbani kwake lakini huwa anakwenda mara kwa mara na
marafiki zake na kwamba aliondoka akamuacha hapo chumbani akiwa na marafiki
zake.
“Lakini
wale marafiki zake saba tuliowakuta nyumbani kwa baba yake mahali ambako
anaishi huyo kijana wakiwa wanavuta bangi wameeleza kuwa ni kweli huyo mtoto
alipotoroka shule ule usiku alikwenda kwa huyo kijana wakawa wote kabla ya
kutoweka kusikojulikana,
“Na
wale waliomsindikiza kwenda kwenye hiyo nyumba ambao ni wanafunzi wenzake nao
tuimewahoji na wanakiri kuwa mtoto Labna alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
huyo kijana na kwamba siku hiyo walimsindikiza akaenda kwake.
“Sasa
unajua wanafunzi wengi wa kidato cha nne wako kwenye mitahani, tunasubiri
jumatano wamalize ili tuiwakutanishe pamoja wote tuliowahoji watueleze kwa
pamoja ndipo tuchukua hatua zaidi,” alisema Kapere.
Alipoulizwa
hatua zitakazochikuliwa na timu hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake
alisema itaandika taarifa itakayoipeleka kwa Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya
kuchukua hatua zaidi lakini itaomba Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Idara
ya Usalama wa Taifa (TISS) vialikwe kusaidia kumsaka mwanafunzi huyo kutokana
na jeshi la polisi kutopata mafanikio.
“Sisi
tutaandika taarifa yetu na tumeishaanza kuandika, tutaeleza upungufu wote
tulioubaini kwenye hiyo shule na tutatoa mapendekezo tutapeleka kwa mkuu wa
wilaya ambaye ndiye aliyeunda timu hii. Lakini niseme tu moja kwa moja katika
mapendekezo yetu tutashauri TISS na JWTZ waalikwe kumsaka huyu mtoto kwasababu
nadhani polisi wanahitaji msaada maana mpaka sasa hawajafanikiwa,” alisema
Kapere.
Mwanafunzi
Labna alitoweka shuleni Oktoba 4, 2020 na taarifa za awali zilieleza kuwa
alitoroka akiwa na wafunzi wanzake kwenda kwenye maeneo ya starehe na kutokomea
moja kwa moja.
Zephania Maduhu ambaye ni mjomba wa mwanafunzi huyo aliyekuwa
akimlipia ada ya shule aliieleza Tanzania PANORAMA Blog kuwa ana wasiwasi mtoto
wake ameuawa kwani tangu Oktoba 4, 2020 alipopotea akiwa chini ya uangalizi wa
shule, taarifa za kupotea kwake zilitolewa Oktoba 8, 2020 na matron wake, Sarah
Murra aliyempigia simu mama mzazi wa mwanafunzi huyo akiulizia kama ameishafika
nyumbani jambo ambalo limekuwa liibua hisia zinazotia shaka kuhusu usalama wa mtoto
huyo.
“Huyo mtoto ninamlea mimi, ninamlipia ada ya shule mimi, ni mtoto wa dada yangu, anasoma St. Mary’s, Mbezi Makonde. Oktoba 8, mwaka huu, matron wake anaitwa Sarah Murra, alimpigia simu mama yake, yaani dada yangu akimuuliza kama Labna kafika nyumbani.
No comments:
Post a Comment