banner

Monday, November 9, 2020

WANAFUNZI WASICHANA ST MARY’S WATOROKA USIKU, MMOJA ATOWEKA

 


NA CHARLES MULLINDA

WANAFUNZI wasichana wa Shule ya Sekondari ya St. Mary’s iliyoko Mbezi Makonde Jijini Dar es Salaam wametoroka shuleni usiku kwenda mahali kusikojulikana huku mmoja akitoweka moja kwa moja.

Taarifa za uhakika zilizoifikia Tanzania PANORAMA Blog zimeeleza kuwa wanafunzi hao walitoroka shuleni wakiwa kundi na kurejea alfajili huko mmoja wao akitokomea mahali kusikojulikana.

Uchunguzi wa Tanzania PANORAMA umebaini kuwa tukio hilo lilitokea mwezi uliopita na mwanafunzi aliyetoweka anasoma kidato cha tatu lakini uongozi wa shule na bodi ya shule wamekuwa wakifanya jitihada kubwa za kuficha tukio hilo na hajawatoa taarifa polisi za kutoweka kwa mwanafunzi huyo.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Dallas Mhoja alipoulizwa na Tanzania PANORAMA alisema kupotea kwa mwanafunzi huyo akiwa shuleni kunamuhusu mkuu wa shule, siyo bodi.

“Wewe vipi bwana, unajua kuwa mimi ni mwenyekiti wa bodi? Sasa kupotea kwa mwanafunzi kunanihusu nini mimi? Mpigie mkuu wa shule muulize huyo ndiye anakaa na hao watoto,. Mimi nashughulika na mambo makubwa ya shule siyo suala na mtoto mmoja kupotea,” alisema Dallas.

Alipoelezwa kuwa taarifa za mwanafunzi kupotea akiwa mikononi mwa uongozi wa shule na shule kutotoa taarifa polisi kwa zaidi ya mwezi mmoja ni kubwa ikizingatiwa mpaka sasa hajapatikana alisema akipata nafasi atafuatilia kwa mwalimu.



Tanzania PANORAMA ilimweleza Mhoja kuwa imefanya uchunguzi wa kina kuhusu kupotea kwa mwanafunzi huyo na inazo taarifa kuwa suala hilo limekwishafikishwa kwake lakini hajachukua hatua yoyote alisisitiza kuwa kwa wadhfa wake wa mwenyekiti wa bodi hastahili kufuatilia mambo ya wasichana wanaotoroka shule usiku na kupotelea wanakokujua hivyo aulizwe mkuu wa shule.

“Aisee we mwandishi mbona una maswali ya kuudhi? Nakwambia hayanihusu mambo wewe umeng’ang’ania kunibana tu unataka nini? Mwenyekiti wa bodi na kupotea kwa mtoto mmoja wanahusianaje?

“ Mimi ni mwenyekiti wa bodi sihusika na kuangalia watoto shuleni tena wanaotoroka shuleni usiku kwenda kwenye mambo yao? Halafu wananogewa huko hawarudi? Muulize mkuu wa shule ndiye anayehusika na malezi ya watoto,” alisema Mhoja.

Alipotafutwa mkuu wa shule kupitia simu yake ya kiganjani, iliita bila kupokelewa.  

Friday, November 6, 2020

MWANASHERIA BAKHRESA ASIMAMIA MKATABA WA KASHFA YA UNYANYASAJI WA KINGONO

 


NA CHARLES MULLINDA

MKATABA wa kuvunja uhusiano binafsi wa wapenzi wawili unaodaiwa kughubikwa na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono uliandaliwa na kusainiwa mbele ya mwanasheria wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (BSS)

Uchunguzi wa Tanzania PANORAMA umebaini kuwa mkataba huo uliandaliwa na kusainiwa ili kuvunja uhusiano wa kimapenzi baina ya Idi Mzee ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya BSS na mwanamke mpenzi wake ambaye jina lake limehifadhiwa.

Imebainika kuwa mwanamke huyo alikwenda kwa mwanasheria wa BSS kumlalamikia Idi kwa kutomlipa ujira wa kazi aliyokuwa amempa ya kufanya tendo la ndoa na wanaume tofauti tofauti huku yeye akitazama kabla ya kushiriki naye pia.

Kwamba mwanamke huyo alidai kuwa alikuwa akichukua wanaume tofauti kwenda kushiriki nao tendo la ndoa mbele ya Idi kwa makubaliano waliyokuwa wamefikia na Idi kuwa watakuwa wakiwalipa lakini katika hatua ya kushangaza Idi alianza kuchelewesha malipo hayo.

“Mwanasheria huyo alimuita Idi na kumuuliza kama anamfahamu huyo mwanamke akakubali, akamuuliza kama madai ya mwanamke huyo kuwa alimpa maelekezo ya kutafuta wanaume na kuwapeleka kwake kushiriki nao tendo la ndoa kabla ya kushiriki naye pia akakubali lakini alisema anataka waachane.

“Ndiyo mwanasheria akaandaa mkataba wa kuwaachanisha kwa makubaliano kuwa Idi alimlipe huyo mwanamke shilingi milioni mbili kisha kila mtu aendelee na maisha yake, ajabu wiki mbili baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Idi alimpigia simu huyo mwanamke akimuomba amtumie picha zake chafu ili aweze kufanya jambo lake kwa ahadi kuwa atamlipa lakini alipotumiwa hakumlipa ndiyo mgogoro ukaanza upya.

“Tatizo hapo ni pesa, yule Idi anatumia pesa nyingi anazodai kuzitoa kwa bosi wake ambaye huwa anamfanyia kazi maalumu na hawa dada zetu wana njaa sana ndiyo maana wanaharibu kabisa maadili yetu, wanahatarisha maisha yao na ya wengine na wanachafua majina ya kampuni zao na mabosi wao.

“Na ajabu hizi sheria nazo zinaruhusu mambo mabaya mno kwa sababu mwanasheria kusimamia makubaliano ya kisheria kwa mtu anayedai mpaka aliyefanyishwa kitendo hicho na mbwa nadhani si sawa,” alisema mtoa taarifa wa Tanzania PANORAMA.

Wakati haya yakibainika, tayari Jeshi la Polisi limeeleza kuwa linasubiri uchunguzi wa kitaalamu wa simu za mkononi za Idi Mzee na mpenzi wake anayemtuhumu kumnyanyasa kingoni pamoja na kumfanyisha tendo la ndoa na mbwa ili hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa.

Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, Jumanne Mkwama ameiambia Tanzania PANORAMA kuwa kinachochunguzwa na polisi ni nani kati ya wawili hao aliyevunja mkataba wa kuvunja uhusiano wa kimapenzi ambao ulisainiwa baada ya kutoelewana kwao.

Alisema mambo mengine yanayolalamikiwa na mwanamke huyo dhidi ya Idi, yatashughulikiwa na mahakama.

Thursday, November 5, 2020

JESHI LA POLISI LASUBIRI UCHUNGUZI WA SIMU TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO KAMPUNI YA BAKHRESA

 


NA CHARLES MULLINDA

JESHI la Polisi linasubiri uchunguzi wa kitaalamu wa simu za mkononi
za Idi Mzee na mpenzi wake wa kike (jina limehifadhiwa) anayemtuhumu kumnyanyasa kingoni pamoja na kumfanyisha tendo la ndoa na mbwa.

Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, Jumanne Mkwama ameiambia Tanzania PANORAMA kuwa uchunguzi huo
utakapokamilika ndipo  hatua nyingine zitafuata.

Kamanda Mkwama amesema kinachochunguzwa na polisi ni nani kati ya
wawili hao aliyevunja mkataba wa kuvunja uhusiano wa kimapenzi ambao
ulisainiwa baada ya kutoelewana kwao.

Alisema mambo mengine yanayolalamikiwa na mwanamke huyo dhidi ya Idi, ikiwemo kumfanyisha tendo la ndoa na mbwa pamoja na kukiuka makubaliano ya kumlipa kila anapofanya tendo la ndoa na mwanaume huku yeye akiangalia kabla ya kushiriki naye tendo hilo yatashughulikiwa na mahakama.

“Tunasubiri uchunguzi wa kitaalamu katika simu zao. Simu zao tumezipeleka kwa wataalamu, tunataka kujua ni nani kati yao aliyevunja mkataba walioingia kwa maandishi wa kuachana. Hayo mengine watajuana wenyewe mahakamani,” aliema Kamanda Mkwama.

Idi Mzee ambaye ni dereva wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB)
amefunguliwa jalada la uchunguzi katika Kituo cha Polisi Chang’ombe
Jijini Dar es Salaam akidaiwa kumshawishi kwa pesa nyingi mwanamke
mmoja aliyekuwa akifanya kazi ya uhudumu katika Baa ya Valle In iliyopo Chang’ombe ili afanye tendo la ndoa na wanaume mbalimbali kabla ya kushiriki naye tendo hilo.

Taarifa hizi zimethibitishwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo
waliofikiwa kwa mahojiano na Tanzania PANORAMA akiwemo mwanasheria na
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bakhresa Food and Beverage (BFB)
Rose Mtesigwa.

Katika mahojiano hayo yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake Kariakoo,
Mtesigwa alianza kwa kueleza kuwa hamfahamu Idi Mzee na hana
kumbukumbu ya kusikia jina hilo mahali popote wala mtu huyo kufanya
kazi katika Kampuni ya Bakhresa.

Baadaye alisema Idi anayemfahamu yeye ameajiriwa katika Kampuni ya
Said Salim Bakhresa (SSB) lakini yeye anasimamia wafanyakazi wa Kampuni ya
Bakhresa Food and Beverage (BFB) na kuelekeza akaulizwe SSB.

“Hiyo Skendo naifahamu vizuri sana na hata chanzo chenu cha taarifa nakifahamu sana sana tu. Mimi hapa ni HR na wakili wa kampuni pia lakini Idi sinaye mimi hapa, yeye yupo SSB. Nendeni pale mapokezi nampa maelekezo dada hapo chini atawapa namba za HR wa SSB yeye ndiyo anaweza kumzungumzia,” alisema Mtesigwa.

Mfanyakazi wa mapokezi makao makuu ya makampuni ya Bakhresa aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Abdalla alitoa namba kama ilivyoelekezwa na Mtesigwa lakini namba hiyo imekuwa ikiita bila kupokelewa.

Awali, Mariam Abdalla naye aliieleza Tanzania PANORAMA kuwa analifahamu suala hilo lakini alishangaa ni nani aliyelifikisha kwa waandishi wa habari.

“Dah! naona sasa siri za kampuni zimeanza kutoka nje. Lakini nawashukuru ninyi ni waungwana sana kwa sababu mmekuja kuutafuta ukweli japo inaonekana mmefikishiwa kila kitu. Ninyi ni wanaume bhana lichukulieni hili jambo kama wanaume. Haya ni kweli yapo na sisi tumekuwa tukisema siku yakitoka nje tutaaibika sana.

“Sasa ujue Idi ni dreva wa mzee Bakhresa mwenyewe kabisa, kweli nawashukuru kwa kupoteza muda wenu kuja walau kupata maelezo ya upande wa pili lakini nataka niwaombe kitu, mimi Idi mtu wangu sana, niacheni nimtafute maana siyo rahisi kumpata kwa sababu simu zake ziko polisi, mpaka saa nane nitakuwa nimempata ili naye kama mlivyo sema aje aseme ilikuwaje kuwaje kwa sababu yapo madai ya kweli ambayo siyo siri yanafahamika lakini kuna mengine huyo mwanamke katia chumvi sana,” alisema Mariam.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Amon Kakwele hakuwa
tayari kulizungumzia suala hilo baada ya kupigiwa simu mara kadhaa
iliyokuwa ikipokelewa na msaidizi wake ambaye alipopokea mara ya
mwisho alisema bosi wake amemtaka mwandishi afike ofisini kwake
kuzungumzia suala hilo badala ya kupiga simu.


Wednesday, November 4, 2020

KAMPUNI YA BAKHRESA YATIKISWA NA KASHFA YA UNYANYASAJI WA KINGONO

 



NA CHARLES MULLINDA

KAMPUNI ya vinywaji ya Mfanyabiashara Bilionea, Said Salim Bakhresa (SSB) imeanza kuandamwa na kashfa za unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanywa na wasaidizi wa karibu wa mfanyabiashara huyo.

Taarifa za uhakika zilizoifikia Tanzania PANAROMA Blog kutoka vyanzo mbalimbali vilivyo ndani ya kampuni hiyo na kuthibitishwa na maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi, zimeeleza kuwa tayari jalada la uchunguzi kuhusu moja ya kashfa hizo limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Changómbe, kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Taarifa hizo za kikachero zimemtaja moja kwa moja, Idi Mzee ambaye ni dreva wa Bilionea Said Bakhresa kuwa ndiye aliyefunguliwa jalada hilo la uchunguzi na kwamba simu zake za kiganjani pamoja na ya mlalamikaji zinashikiliwa na polisi kwa uchunguzi.

Inadaiwa kwamba mtuhumiwa alimshawishi kimapenzi kwa ukwasi mkubwa wa fedha mwanamke aliyekuwa akifanya kazi baa ya Valle Inn (jina tunalihifadhi) iliyopo Changómbe, Dar es Salaam kabla ya kumpa masharti magumu.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mwanamke huyo zimedai kuwa Idi Mzee alimtaka mwanamke huyo awe anakutana naye akiwa na mwanamme aliyemuandaa kwa ajili ya kufanya naye tendo la ndoa huku yeye akitazama na wakimaliza ndipo Idi naye hufanya tendo hilo na mwanamke huyo huyo.

“Hii kesi ya watu Bakhersa na huyo dada (anamtaja jina)kweli ipo polisi. Yule mwanamke kamshtaki Idi kwa unyanyasaji wa kingono lakini kwa pia kwa kumfanyisha mapenzi na mbwa. Tatizo polisi wa Changómbe hata sijui kama mtaifuatilia watawapa ushirikiano si unajua tena inahusu ofisi ya mtu mkubwa.

“Yule Idi ana tatizo fulani linalofahamika kwa wafanyakazi wenzake wote na muhusika wake ambaye ni mkubwa wa pale pale anafahamika kwa hiyo hawezi kufanya tendo la ndoa mpaka kwanza aone wengine wanafanya ndiyo na yeye anaweza kufanya.

“Sasa alimwambia yule mwanamke awe anatafuta wanaume anawapa pesa anakwenda nao kwake wanashiriki naye wakimaliza ndiyo Idi naye anashiriki na mwanamke huyo. Baada akaanza kumwambia leo njoo na mzee sana, mara njoo na kivulana cha shule na kwa vile ana pesa na yeye anasema pesa hiyo anapewa na mtu wake Bakhresa, hakuna mtu mwenye njaa anayeweza kukataa.

“Katembea na wanaume wengi sana huyo dada aliokwenda nao kwa Idi na kama ni ugonjwa sijui wangapi wameambukizwa Mungu apishilie mbali, na hao wanaume aliotembea nao wamekwenda polisi wamehojiwa na wamekubali kuwa ni kweli walikuwa wanafanya naye hayo matendo machafu mbele ya Idi na hadi mbwa kaishawahi kumuingilia huyo dada mbele ya Idi. Sasa wanapambana kuizima hao wakubwa na ndiyo tunasubiri kauli ya polisi,”kileleza chanzo cha Habari.

Alipoulizwa jana Mlinzi Mkuu wa SSB, Charles Zuakuu kuhusu kashfa hiyo alibabaika kujibu ambapo alianza kusema hasikii vizuri anachoulizwa kisha akakata na kuzima kabisa simu yake.

Alipopigiwa baadaye alitaka kwanza atajiwe jina  la mtu aliyevujisha siri hiyo na jina la mlalamikaji huku akikiri kuwa ni kweli Idi Mzee ni dreva wa Said Bakhresa.

Alipoulizwa leo Meneja Rasilimali Watu aliyejitambulika kwa jina la Rose Mtesigwa kuhusu kashfa hiyo naye alianza kwa kubabaika alipoeleza kuwa hamfahamu kabisa Idi Mzee na hana kumbukumbu ya kusikia jina lake mahali popote wala kufanya kazi katika Kampuni ya Bakhresa.

Alipoelezwa kuwa lengo la Tanzania PANORAMA kuhoji ni kutaka kuthibitisha iwapo ndiye anayechunguzwa na polisi kwa unyanyasaji wa kingono, Mtesigwa alibadilisha kauli kwa kueleza kuwa Idi anayemfahamu yeye ameajiriwa na Kampuni ya SSB wakati yeye anasimamia wafanyakazi wa Kampuni ya Chakula (BFB)

“Hiyo skendo naifahamu vizuri sana na hata chanzo chenu cha taarifa nakifahamu sana sana tu  mimi hapa ni HR na wakili wa kampuni pia. Lakini Idi sinaye mimi hapa yeye yupo SSB . nendeni pale mapokezi nampa maelekezo dada  hapo chini atawapa namba za HR wa SSB yeye ndiyo ataweza kumzungumzia,” alisema Mtesigwa.

Hata hivyo simu iliyotolewa na mtu wa mapokezi ilipopigwa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Amon Kakwale, alipopigiwa simu yake ilipokelewa na msaizidi wake aliyeeleza kuwa bosi wake yupo kwenye kikao na ilipopigwa tena baadaye alipokea tena msaidizi wake na kueleza kuwa kamanda huyo alimtaka mwandishi kufika ofisi kwake kuzungumzia suala hilo badala ya kupiga simu.                  

 


Monday, November 2, 2020

WAJANJA DAR WAHAMISHIA MAFICHONI VIWANDA VYA MIFUKO YA PLASTIKI ILIYOPIGWA MARUFUKU

 

 


NA MWANDISHI WETU

IMEBAINIKA kuwa baadhi ya  wafanyabiashara jijini Dar es Salaam wanaendelea kutengeneza mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na serikali kutokana na kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.

Uchunguzi waTanzania PANORAMA umebaini kuwepo kwa viwanda hivyo katika makazi ya watu yaliyo nje kidogo ya jiji huku ikiwa haina vibali vyovyote vya uzalishaji wa vifungashio.

Aidha, maeneo vilipo viwanda hivyo kuna walinzi ambao hukaa umbali wa hatua 30 hadi 50 ambao kazi yao ni kuangalia kama kuna watu wanaofutilia uzalishaji au kuchunguza eneo la kiwanda kisha hutoa taarifa kwa walio kiwandani kusimamisha uzalishaji na kufunga kiwanda.

Uchunguzi wa kina wa Tanzania PANORAMA umebaini moja ya kiwanda cha mifuko ya plaskiti kipo eneo la Mbezi Kifuru kwa Richard ambacho mmiliki wake hafiki eneo la kiwanda bali ameweka walinzi wanaompatia taarifa za kila mtu anayefika kiwanda hapo kwa kumpigia simu.

Wakizungumza na Tanzania PANORAMA, wafanyakazi wa kiwanda hicho walisema wanajua wanafanya kazi kwa uficho na katika mazingira magumu lakini wanalazimika kufanya kutokana na ugumu wa maisha.

Msimamizi mkuu wa kiwanda hicho ambaye alikataa kujitambulisha jina lake alieleza kuwa kazi yake ni kuangalia usalama na kumpa taarifa bosi wake ambaye pia ni mjomba wake kuhusu wageni wanaofika kiwanda hapo.

“Kiukweli mimi ni msimamizi ila mjomba ndiye anajua kila kitu  mje wakati mwingine atakapokuwa hapa. Najua hatuna vibali na tunaendesha kiwanda kinyume cha taratibu lakini mkiongea na mjomba yeye anajua kila kitu,” alisema.

Mmiliki wa kiwanda hicho aliyefamika kwa jina la Ali Mbonde alipoongea na Tanzania PANORAMA kwa simu alisema anajua kila kitu lakini jambo hilo linahitaji mazungumzo badala ya kuandikwa kwa sababu litasababisha usumbufu usiokuwa wa lazima.

Tanzania PANORAMA inaendelea na uchunguzi wa sakata hili.