banner

Thursday, October 1, 2020

UTATA WATANDA UINGIZAJI DAWA ZA MIFUGO

 


KAMPUNI ya Multvet Farm Ltd ya jijini Dar es Salaam inadaiwa kuingiza nchini dawa za mifugo na kuzisambaza kwa matumizi kwa kutumia vibali vyenye shaka vya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

Taarifa za uhakika zilizoifikia TANZANIA PANORAMA zimedai kuwa sehemu kubwa ya vifaa hivyo inaagizwa kutoka Afrika Kusini na muagiza amekuwa akilipa kodi zote za serikali lakini katika hatua ya kushangaza amekuwa akitumia vibali vyenye shaka vya TMDA.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Kampuni ya Multvet vimeeleza kuwa mwenendo huo wa kutumia vibali vyenye shaka ni wa muda mrefu tangu TMDA ilipokuwa ikijulikana kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)

TANZANIA PANORAMA limeiona orodha ya baadhi ya vibali na dawa za mifugo zinazoingiwa nchini kwa kutumia vibali vyenye kutiliwa shaka vinaonyesha kutolewa na TFDA

Moja ya kibali kinachodaiwa kuwa na shaka kilicchoonwa na TANZANIA PANORAMA kinaonyesha kilitolewa Juni 17, 2018 kikiwa na namba TFDA - WEB0518/D/IPER/1032 na kilitumika kuingiza dawa za mifugo kutoka nchini Afrika Kusini.

Alipoulizwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo (jina tunalihifadhi) aliyesema yeye siyo msemaji rasmi, kwanza alikanusha kufahamu lolote kuhusu madai hayo lakini alipoelezwa kuwa TANZANIA PANORAMA limeona baadhi ya vibali vinavyodaiwa kutiliwa shaka na dawa ambazo zimekuwa zikiingizwa nchini kwa kutumia vibali vya aina hiyo alisema hayo ni mambo ya zamani na hivi sasa kampuni hiyo ilishaachana nayo.

Alisema hivi sasa yeye na washirika wake wanamiliki kiwanda cha kutengeneza dawa za mifugo lakini alipobanwa kuwa vibali vinavyodaiwa kutumiwa na kampuni yake kuingiza na kumbaza dawa hizo alisema ni kweli jambo hilo liliwahi kutokea na alilipeleka Dodoma kwa wakubwa bila kufafanua alilipeleka kwa wakubwa gani na likichukukiwa maamuzi gani.

Msemaji wa TMDA, Gaudencia Simwaza akizungumzia suala  hilo baada ya TANZANIA PANORAMA kumfikishia alisema taassii yake imelipokea na inaendelea na uchunguzi kabla ya kutoa tamko.

 

WACHINA 'WAOGA' NOTI DAR ES SALAAM



NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI mbili za ujenzi za China, China Road and Breadge Corporation (CRBC) na SCG Overseas Tanzania Company Limited zinadaiwa kufanya biashara inayoziingia mabiilioni ya shilingi ambayo hayatozwi kodi.

Sambamba na biashara hiyo inayoyaingizia utajiri mkubwa lakini unaofubaza fuko la fedha zikusanywazwo na Mamlaka ya Mapato (TRA) kama kodi, Kampuni ya CRBC imekusanya na kutia kibindoni mamilioni ya fedha ilizokuwa ikiwakata wafanyakazi wake kama malipo ya pensheni.

Taarifa za uhakika zilizoifikia TANZANIA PANORAMA zimedai kuwa SCG Overseas Tanzania Company Limited ambayo iliingia nchini kwa ajili ya kujishughulisha na  ujenzi wa barabara na madaraja ilipewa msamaha wa kodi wa vifaa vyake vya ujenzi.

Inadaiwa kampuni hiyo ambayo sasa imemaliza shughuli zake hapa nchini, imekuwa ikikodisha vifaa ilivyokuwa ikitumia kwa shughuli zake  za ujenzi vikiwa na msamaha wa kodi kwa Kampuni ya CRBC ambayo huilipa mamilioni ya fedha.

Taarifa zaidi zilizokusanywa na TANZANIA PANORAMA zimeonyesha kuwa biiashara kati ya kampuni hizo mbili, licha ya kuwa yenye thamani kubwa, risiti zinazotolewa  kuthibitisha kufanyika kwa malipo hazitambuliki kwenye mfumo rasmi wa kikodi wa hapa nchini.

"Hawa wachina wa hizo kampuni mbili wanafanya biashara ya mabilioni kwa kukodishiana vifaa na mitambo ya ujenzi. Kiukweli wanaoga fedha hapa Dar as Salaam," alisema mmoja wa watoa taarifa.

Wakati huo huo, CRBC inadaiwa kuweka katika fuko lake ya fedha mamilioni ya shilingi waliyokuwa wakikatwa wafanyakazi wake kama malipo ya pensheni.

Katika mahojiano kati ya badhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na TANZANIA PANORAMA huku wakiwa na nyaraka zao za malipo ya mshahara mkononi (salary slip) wamedai kwa zaidi ya mwaka mmoja walikuwa wakikatwa pesa katika mishahara yao kwa ajili ya pensheni lakini baada ya mikataba yao ya kazi kuisha wamebaini kuwa fedha hizo zilikuwa haziwasilishwi kwenye mifuko ya jamii.

Alipoulizwa Meneja Rasilimali Watu wa CRBC Alice Charles kuhusu madai hayo alikubali kuzungumzia suala ya malipo ya pensheni huku dai la kuwepo biashara baina ya CRBC na SCG  alisema hilo kwake ni zito na anayeweza kulisemea ni bosi wake aliyemtaja kwa jina moja la Zhang.

Alice alisema madai ya wafanyakazi kukatwa sehemu ya mishahara yao kwa ajili ya pensheni ni ya kweli.

Aidha Alice alieza zaidi kuwa fedha hizo badala ya kuwasilishwa kwenye mifuko ya kijamii zilikuwa zikiingizwa kwenye fuko Kuu la kampuni hiyo kwa sababu wafanyakazi hao walikuwa siyo wanachama wa mifuko hiyo.

Alice aliahidi kuwasiliana na bosi wake Zhang ili azungumzie madai ya kuwepo biashara baina ya CRBC na SCG na kwamba taarifa rasmi angeitoa kwa TANZANIA PANORAMA lakini kwa zaidi ya wiki mbili ameshindwa kutekeleza Ahadi yake hiyo.

Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alipotafutwa kuzungumzia iwapo taratibu za mamlaka hiyo zinaruhusu vifaa vilivyoingizwa nchini vikiwa na msamaha wa kodi kutumiwa kibiashara, simu yake iliita zaidi ya mara tano bila kupokelewa na hata alipotumiwa maswali kwa ujumbe mfupi kwenye simu yake ya kiganjani, aliyasoma lakini hakujibu chochote.

Jitihada za kumpata balozi wa China kuzungumzia hilo hazikiweza kuzaa matunda baada ya simu kuwa inaita bila kupokelewa.

Mwisho. 

Wednesday, September 30, 2020

MAJALIWA: MCHANGUENI DK. MAGUFULI, ANATOKA CHAMA KINACHOJALI WANANCHI

 


*Ampokea aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Kyerwa wamchague Dk. John Pombe Magufuli kuwa rais kwa sababu anatoka katika chama ambacho kina mikakati inayotokana na mawazo ya wananchi.

"Dk. Magufuli anatoka kwenye chama ambacho kina utaratibu katika kuendesha nchi, chama ambacho kina ratibu kero za wananchi, ambacho kinasikiliza wananchi mpaka ngazi ya chini," amesema.

Ametoa wito huo leo (Jumanne, Septemba 29, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nkwenda, akiwa njiani kuelekea Isingiro wilayani Kyerwa, mkoani Kagera.

"Tumemjaribu na amefanya mambo makubwa katika wizara alizoziongoza na ndiyo maana namleta kwenu Dk. Magufuli na kumuombea miaka mingine mitano ili alete maendeleo zaidi," amesema.

Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kyerwa, Innocent Bilakwate, mgombea udiwani wa Kata ya Nkwenda, Edward Katunzi na wagombea wa CCM wa kata za jirani.

Amesema CCM ni chama kinachoongozwa na Ilani ya Uchaguzi na kuna mambo yamethibitika katika ilani inayoishia 2020.

"Leo tunaleta kitabu kingine cha Ilani ya 2020 - 2025. Kama tuliweza kufanya makubwa ndani ya miaka mitano na kile kitabu kidogo, je huko tuendako itakuwaje?"  amesema.

Akiwa Isingiro kwenye mkutano wa hadhara, Majaliwa amesema serikali ilibadilisha sheria tangu mwaka 2017 na ikazuia uuzaji wa madini ya bati nje ya nchi kwa kutumia njia za panya.

"Sheria inatutaka tutenge ekari kadhaa kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Leo hii ekari 38,000 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini mbalimbali. Pia tumeanzisha masoko ya madini 26 na vituo vidogo 28 vya kuuzia madini," amesema.

 Akifafanua kuhusu vitambulisho vya Taifa, Majaliwa amesema Tanzania ni nchi ya amani na wengi wanatamani kuja kuishi nchini.

Amesema Wilaya za Kyerwa, Karagwe na Missenyi ni za mipakani kwa hiyo zina changamoto za uhamiaji na masuala ya kiraia.

"Ndiyo maana serikali inakuwa makini katika uhakiki. Tutaimarisha usimamizi ili kila Mtanzania apate kitambulisho," amesema.

Pia amewaonya maafisa wanaohusika na utaoaji vitambulisho vya uraia ambao wanapokea hongo na kuwapa vitambulisho hivyo watu wasiostahili.

Wakati huohuo, Majaliwa amempokea aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Karagwe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Princepius Rwazo ambaye ameamua kurejea CCM. 

Akizungumza kwenye mkutano huo, Rwazo amesema alikuwa mgombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu uliopita na aliisumbua sana CCM lakini sasa ameamua kurejea kwani ameona mazuri yanayofanywa na chama hicho.

"CCM imejibu kiu zetu, kimekuwa kama chama cha upinzani, na wapinzani sasa wamelala. Nimerudi CCM, sihitaji cheo chochote, shida yangu ni kujiunga na watu wanaochapa kazi. Nitamuunga mkono Dk. Magufuli na ndugu yangu Bashungwa," amesema na kushangiliwa.

Majaliwa anaendelea za ziara yake katika Wilaya za Karagwe na Missenyi.

MAJALIWA: SERIKALI YATEKELEZA MIRADI 1,423 YA MAJI

 


Kayanga ni miongoni mwa miji 28 iliyonufaika na sh. tril. 1.2 za miradi hiyo

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa amesema Serikali imetekeleza miradi ya maji 1,423 ikiwemo mradi wa kupeleka maji kwenye miji 28 inayotekelezwa kwa sh. trilioni 1.2.

“Kayanga imepata sh. bilioni 58, ni miongoni mwa miji 28 iliyopata fedha za mradi wa maji kitaifa ambao unajumuisha mikoa mingi,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 29, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kayanga, katika mikutano uliofanyika kwenye uwanja wa Changarawe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera.

Mikoa inayohusika na mradi huo miji yake kwenye mabano ni Tanga (Handeni/Korogwe, Muheza na Pangani); Njombe (Njombe, Wanging’ombe na Makambako); Kagera (Kayanga); Mtwara (Nanyumbu na Makonde) na Singida (Manyoni).

Pia Ruvuma (Songea); Tabora (Sikonge, Urambo-Kaliua); Mbeya (Rujewa na Chunya); Kigoma (Kasulu); Lindi (Kilwa Masoko); Mara (Mugumu, Rorya/Tarime); Geita (Geita na Chato); Singida (Singida Mjini na Kiomboi); Katavi (Mpanda); Dodoma (Chamwino na Chemba); Iringa (Mafinga); na Morogoro (Ifakara).

Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, mgombea udiwani wa Kata ya Kayanga, na wagombea wa CCM wa kata za wilaya hiyo.

Amesema miradi mingine ya maji inayotekelezwa kwenye wilaya hiyo imetumia sh. bilioni 5.2 kwa ajili ya uboreshaji wa miradi ya maji. Ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa maji Kijiji cha Nyaishozi ambao umetumia sh. milioni 706, umekamilika na unatoa huduma.

“Shilingi bilioni 1.6 zilitumika kwa ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Chamchuzi, mradi umekamilika na unatoa huduma, shilingi milioni 805 zilitumika kwa ujenzi wa mradi wa maji Chanika, mradi umekamilika na unatoa huduma," amesema.

Amesema sh. milioni 63 zilitumika kwa uchimbaji wa visima vinne na ufungaji wa pampu katika vijiji vya Okakajinja na Chonyonyo, mradi ambao umekamilika na unatoa huduma. 

Amesema fedha nyingine zilizotumika ni sh. milioni 120 kwa ajili ya mradi wa maji uchimbaji wa visima vinne na ufungaji wa pampu katika vijiji vya Mulamba na Nyarugando, ambao pia umekamilika na unatoa huduma.

Amesema sh. bilioni 2.4 zilitumika kwa ajili ya mradi wa maji Nyakakika, ambao uko katika hatua za umaliziaji na sh. milioni 251 zilitumika kwa ajili ya mradi wa maji Rugu, ambao nao upo kwenye hatua za majaribio.

CHADEMA CHANYOOSHEWA KIDOLE KWA MAUAJI YA KIKATILI

 


NA MWANDISHI WETU

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshutumiwa kuhusika moja kwa moja na tukio la mauaji ya kinyama ya kijana Bryan Mollel.

Kwa mujibu wa taarifa ya kulaani mauaji hayo liyotolewa na Katibu Msaidizi wa Taasisi ya Amani na Maendeleo (TAMA), Mkoa wa Songwe, Jackson Eliabu inawataja waliohusika na mauaji ya kikatili ya kijana Mollel kuwa ni viongozi wa Chadema ambao walimpondaponda kwa mawe hadi alipokufa.

Taarifa ya Eliabu  inawataja wagombea udiwani wa Chadema wa Mkoa wa Songwe kuongoza mauaji hayo kwa sababu ya kulazimisha wapewe fomu nyingine baada ya kuharibu waliyokuwa nayo.

Sehemu ya taarifa hiyo inasomeka hivi; 'Tumepokea kwa masikitiko mauaji yaliyofanywa na kuongozwa na wagombea wa udiwani wa Chadema mkoani Songwe waliyoyafanya hivi karibuni kisa kulazimisha kupewa fomu nyingine baada ya kuharibu fomu ya awali.

'Taarifa zinaeleza kijana Bryan Mollel aliuawa na wafuasi na viongozi wa Chadema baada ya juhudi zao za kuhonga hela ili waruhusiwe kuendelea kugombea kushindikana.'

Taarifa ya Eliabu inaeleza zaidi kuwa mbali ya kutekeleza mauaji hayo ya kinyama ya Mollel, pia walitaka kumuua kijana mwingine ambaye aliokolewa na polisi akiwa ameikwishambuliwa na sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

'Mbali na kumpondaponda kwa mawe pia walitaka kumuua kijana mwingine kabla hajaokolewa na polisi na sasa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya akiwa na hali mbaya.' inasomeka taarifa hiyo.

Taarifa hii ya Eliabu ni mwendelezo ya madai ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakikihusisha Chadema na baadhi ya makada wake na mauaji wakiwemo viongozi wa juu.

Freeman Mbowe alipata kunyooshewa kidole  akihusishwa na kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Zakayo Wangwe kilichotokea eneo la Pandambili mkoani Dodoma na alinusurika kushambuliwa na wananchi wa Tarime alipokwenda kuhudhuria mazishi yake.

Aidha,  Chadema kimekuwa kikihusishwa na matukio mbalimbali ya mauaji katika shughuli zake za kisiasa ikiwemo mikutano na maandamano