banner

Wednesday, November 4, 2020

KAMPUNI YA BAKHRESA YATIKISWA NA KASHFA YA UNYANYASAJI WA KINGONO

 



NA CHARLES MULLINDA

KAMPUNI ya vinywaji ya Mfanyabiashara Bilionea, Said Salim Bakhresa (SSB) imeanza kuandamwa na kashfa za unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanywa na wasaidizi wa karibu wa mfanyabiashara huyo.

Taarifa za uhakika zilizoifikia Tanzania PANAROMA Blog kutoka vyanzo mbalimbali vilivyo ndani ya kampuni hiyo na kuthibitishwa na maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi, zimeeleza kuwa tayari jalada la uchunguzi kuhusu moja ya kashfa hizo limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Changómbe, kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Taarifa hizo za kikachero zimemtaja moja kwa moja, Idi Mzee ambaye ni dreva wa Bilionea Said Bakhresa kuwa ndiye aliyefunguliwa jalada hilo la uchunguzi na kwamba simu zake za kiganjani pamoja na ya mlalamikaji zinashikiliwa na polisi kwa uchunguzi.

Inadaiwa kwamba mtuhumiwa alimshawishi kimapenzi kwa ukwasi mkubwa wa fedha mwanamke aliyekuwa akifanya kazi baa ya Valle Inn (jina tunalihifadhi) iliyopo Changómbe, Dar es Salaam kabla ya kumpa masharti magumu.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mwanamke huyo zimedai kuwa Idi Mzee alimtaka mwanamke huyo awe anakutana naye akiwa na mwanamme aliyemuandaa kwa ajili ya kufanya naye tendo la ndoa huku yeye akitazama na wakimaliza ndipo Idi naye hufanya tendo hilo na mwanamke huyo huyo.

“Hii kesi ya watu Bakhersa na huyo dada (anamtaja jina)kweli ipo polisi. Yule mwanamke kamshtaki Idi kwa unyanyasaji wa kingono lakini kwa pia kwa kumfanyisha mapenzi na mbwa. Tatizo polisi wa Changómbe hata sijui kama mtaifuatilia watawapa ushirikiano si unajua tena inahusu ofisi ya mtu mkubwa.

“Yule Idi ana tatizo fulani linalofahamika kwa wafanyakazi wenzake wote na muhusika wake ambaye ni mkubwa wa pale pale anafahamika kwa hiyo hawezi kufanya tendo la ndoa mpaka kwanza aone wengine wanafanya ndiyo na yeye anaweza kufanya.

“Sasa alimwambia yule mwanamke awe anatafuta wanaume anawapa pesa anakwenda nao kwake wanashiriki naye wakimaliza ndiyo Idi naye anashiriki na mwanamke huyo. Baada akaanza kumwambia leo njoo na mzee sana, mara njoo na kivulana cha shule na kwa vile ana pesa na yeye anasema pesa hiyo anapewa na mtu wake Bakhresa, hakuna mtu mwenye njaa anayeweza kukataa.

“Katembea na wanaume wengi sana huyo dada aliokwenda nao kwa Idi na kama ni ugonjwa sijui wangapi wameambukizwa Mungu apishilie mbali, na hao wanaume aliotembea nao wamekwenda polisi wamehojiwa na wamekubali kuwa ni kweli walikuwa wanafanya naye hayo matendo machafu mbele ya Idi na hadi mbwa kaishawahi kumuingilia huyo dada mbele ya Idi. Sasa wanapambana kuizima hao wakubwa na ndiyo tunasubiri kauli ya polisi,”kileleza chanzo cha Habari.

Alipoulizwa jana Mlinzi Mkuu wa SSB, Charles Zuakuu kuhusu kashfa hiyo alibabaika kujibu ambapo alianza kusema hasikii vizuri anachoulizwa kisha akakata na kuzima kabisa simu yake.

Alipopigiwa baadaye alitaka kwanza atajiwe jina  la mtu aliyevujisha siri hiyo na jina la mlalamikaji huku akikiri kuwa ni kweli Idi Mzee ni dreva wa Said Bakhresa.

Alipoulizwa leo Meneja Rasilimali Watu aliyejitambulika kwa jina la Rose Mtesigwa kuhusu kashfa hiyo naye alianza kwa kubabaika alipoeleza kuwa hamfahamu kabisa Idi Mzee na hana kumbukumbu ya kusikia jina lake mahali popote wala kufanya kazi katika Kampuni ya Bakhresa.

Alipoelezwa kuwa lengo la Tanzania PANORAMA kuhoji ni kutaka kuthibitisha iwapo ndiye anayechunguzwa na polisi kwa unyanyasaji wa kingono, Mtesigwa alibadilisha kauli kwa kueleza kuwa Idi anayemfahamu yeye ameajiriwa na Kampuni ya SSB wakati yeye anasimamia wafanyakazi wa Kampuni ya Chakula (BFB)

“Hiyo skendo naifahamu vizuri sana na hata chanzo chenu cha taarifa nakifahamu sana sana tu  mimi hapa ni HR na wakili wa kampuni pia. Lakini Idi sinaye mimi hapa yeye yupo SSB . nendeni pale mapokezi nampa maelekezo dada  hapo chini atawapa namba za HR wa SSB yeye ndiyo ataweza kumzungumzia,” alisema Mtesigwa.

Hata hivyo simu iliyotolewa na mtu wa mapokezi ilipopigwa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Amon Kakwale, alipopigiwa simu yake ilipokelewa na msaizidi wake aliyeeleza kuwa bosi wake yupo kwenye kikao na ilipopigwa tena baadaye alipokea tena msaidizi wake na kueleza kuwa kamanda huyo alimtaka mwandishi kufika ofisi kwake kuzungumzia suala hilo badala ya kupiga simu.                  

 


Monday, November 2, 2020

WAJANJA DAR WAHAMISHIA MAFICHONI VIWANDA VYA MIFUKO YA PLASTIKI ILIYOPIGWA MARUFUKU

 

 


NA MWANDISHI WETU

IMEBAINIKA kuwa baadhi ya  wafanyabiashara jijini Dar es Salaam wanaendelea kutengeneza mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na serikali kutokana na kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.

Uchunguzi waTanzania PANORAMA umebaini kuwepo kwa viwanda hivyo katika makazi ya watu yaliyo nje kidogo ya jiji huku ikiwa haina vibali vyovyote vya uzalishaji wa vifungashio.

Aidha, maeneo vilipo viwanda hivyo kuna walinzi ambao hukaa umbali wa hatua 30 hadi 50 ambao kazi yao ni kuangalia kama kuna watu wanaofutilia uzalishaji au kuchunguza eneo la kiwanda kisha hutoa taarifa kwa walio kiwandani kusimamisha uzalishaji na kufunga kiwanda.

Uchunguzi wa kina wa Tanzania PANORAMA umebaini moja ya kiwanda cha mifuko ya plaskiti kipo eneo la Mbezi Kifuru kwa Richard ambacho mmiliki wake hafiki eneo la kiwanda bali ameweka walinzi wanaompatia taarifa za kila mtu anayefika kiwanda hapo kwa kumpigia simu.

Wakizungumza na Tanzania PANORAMA, wafanyakazi wa kiwanda hicho walisema wanajua wanafanya kazi kwa uficho na katika mazingira magumu lakini wanalazimika kufanya kutokana na ugumu wa maisha.

Msimamizi mkuu wa kiwanda hicho ambaye alikataa kujitambulisha jina lake alieleza kuwa kazi yake ni kuangalia usalama na kumpa taarifa bosi wake ambaye pia ni mjomba wake kuhusu wageni wanaofika kiwanda hapo.

“Kiukweli mimi ni msimamizi ila mjomba ndiye anajua kila kitu  mje wakati mwingine atakapokuwa hapa. Najua hatuna vibali na tunaendesha kiwanda kinyume cha taratibu lakini mkiongea na mjomba yeye anajua kila kitu,” alisema.

Mmiliki wa kiwanda hicho aliyefamika kwa jina la Ali Mbonde alipoongea na Tanzania PANORAMA kwa simu alisema anajua kila kitu lakini jambo hilo linahitaji mazungumzo badala ya kuandikwa kwa sababu litasababisha usumbufu usiokuwa wa lazima.

Tanzania PANORAMA inaendelea na uchunguzi wa sakata hili.      

Saturday, October 31, 2020

MAJALIWA AKABIDHIWA CHETI CHA UBUNGE RUANGWA

 

 



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti cha ushindi wa Ubunge wa Jimbo la Ruangwa kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Frank Chonya (kushoto)  kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya  ya Ruangwa, Oktoba 29, 2020. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)


MWANDISHI WETU

MBUNGE Mteule wa Jimbo la Ruangwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea cheti cha kumtambulisha rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.

Alipokea cheti hicho Alhamisi, Oktoba 29, 2020 kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ruangwa, Frank Chonya katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.

Akizungumza mara baada ya kupokea cheti hicho, Majaliwa amesema anamshukuru Mungu kwa kuwezesha yote na kuwafikisha hapo na kuwavusha salama kipindi cha kampeni kwa karibu miezi miwili

Majaliwa ambaye alikuwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, alisema kipekee anashukuru vyama vya siasa wilayani humo kwa kumuamini na kuthamini maendeleo.

"Sisiti kusema vyama vya siasa vimeendelea kuthamini maendeleo ya wilaya yetu. Lakini katika hili, niseme kwamba tumeliweka mbele sana suala la maendeleo ya wilaya yetu. Ninawashukuru sana."

Alisema kupatiwa cheti cha kumtambua rasmi kuwa mbunge mteule hadi atakapoapishwa, kumetokana na imani yao kubwa waliyoionesha kwake na kuamua apite bila kupingwa.

"Leo niko hapa mbele yenu, nimemaliza muda wangu wa 2015-2020, mmenivumilia, mmenipa ushirikiano na mmenisaidia kuifanya kazi yangu vizuri. Ninawashukuru viongozi wote na wananchi wa Ruangwa kwa mchango wenu uliowezesha Ruangwa ipige hatua ya maendeleo. Mimi, mke wangu na watoto tunawashukuru sana."

Alisema katika miaka mitano iliyopita, yako mambo mengi waliyofanya na katika kipindi hiki yako mambo yaliyobakia kama kupeleka umeme na maji vijijini. "Ninawaahidi kushirikiana nanyi ili kufikia malengo yaliyowekwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM."

Aliwapongeza madiwani wote walioshinda katika kata zote 22 na kuwaahidi kuwa yuko pamoja nao kuijenga Ruangwa.

Mapema, akizungumza kabla ya kumkabidhi cheti chake, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Ruangwa, Frank Chonya alisema jimbo hilo lenye kata 22, lilikuwa na watu waliojiandikisha kupiga kura 106,043 na lilikuwa na vituo 311 vya kupigia kura.

Alisema vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo ni CCM, ACT Wazalendo, CUF na CHADEMA.

"Kabla ya uchaguzi, kata saba, wagombea wake kutoka Chama cha Mapinduzi walipita bila kupingwa. Jana baada ya uchaguzi, CCM imeshinda kata 12, ACT kata mbili na CUF kata moja." Alisema.

 

 

 

  

WAZIRI MKUU MAJALIWA APIGA KURA KIJIJINI KWAKE

 


*Asema ameridhishwa na shughuli inavyoendelea

 NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amepiga kura kijijini kwake Nandagala, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge mteule wa jimbo la Ruangwa alipiga kura kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala Jumatano, Oktoba 28, 2020 akiwa na mkewe Mama Mary Majaliwa.

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Waziri Mkuu alisema shughuli ya kupiga kura ni haki ya msingi na anamshukuru Mungu imeenda salama.

“Ninamshukru Mungu nimeweza kushiriki haki yangu ya msingi ya kumchagua kiongozi ninayempenda ili aweze kuliongoza taifa hili.

“Kwa hapa Nandagala, Mbunge na Diwani walishapita bila kupingwa, kwa hiyo leo nimepiga kura moja tu ya kumchagua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Waziri Mkuu Majaliwa aliwasili kituoni saa 4:20, na kujipanga foleni yeye na mkewe, alifuata taratibu kama wananchi wengine na alipiga kura saa 4:53. Aliondoka kituoni hapo saa 5:00 asubuhi.

Akielezea kuhusu utaratibu wa upigaji kura, Majaliwa alisema shughuli zima ilienda vizuri na aliwapongeza wasimamizi wa kituo hicho kwa sababu alikuta kuna utulivu na watu wamekaa kwenye foleni wakisubiri kuingia ndani.

“Nimekuta watu wanafuata utaratibu, wanapatiwa maelekezo, vitambulisho vinahakikiwa, ni jambo la kujivunia. Amani kwetu bado ni tunu ambayo hatutakiwi kuidondosha chini ikaharibika. Ninatoa wito kwa Watanzania tujitokeze tukapige kura ili tupate viongozi wa ngazi zote ambao watatuongoza. Ni nafasi muhimu, ukiikosa leo, hutaipata tena kwa miaka mitano ijayo,” alisema.

Tuesday, October 27, 2020

DK. MAGUFULI APIGA SIMU, AOMBA KURA NACHINGWEA


NA MWANDISHI WETU

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli amepiga simu na kuwaomba wakazi wa Nachingwea wampe kura za ndiyo kesho watakapoenda kupiga kura.

Kesho, Jumatano, Oktoba 28, 2020 ni siku ya uchaguzi mkuu hapa nchini ambapo Watanzania watapata nafasi ya kumchagua Rais, wabunge na madiwani.

Dk. Magufuli ameongea nao leo mchana Jumanne, Oktoba 27, 2020 wakati akizungumza na maelfu ya wakazi wa Nachingwea kupitia simu aliyompigia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Boma katika mkutano uliofanyika viwanja vya Bomani kwenye mji mdogo wa Nachingwea, mkoani Lindi.

Majaliwa leo amehitimisha mikutano ya kampeni ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli kwa kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Nachingwea kupitia CCM, Dk. Amandus Chinguile na wagombea udiwani wa kata za wilaya hiyo.

“Ninawasalimu sana wana-Nachingwea. Zile changamoto za zao la korosho, ninazijua; zile changamoto za barabara ninazijua na yote hayo tumeyapanga kwenye Ilani yetu. Nilitamani nifike huko lakini nimemtuma Waziri Mkuu wangu mpendwa aje kuniombea kura, yote atakayoyasema ni ya kwangu. Baada ya uchaguzi, nitakuja kuwaona.

“Nawaombeni kura zenu nyingi, nawaomba mumchague mbunge wa CCM na madiwani wa CCM ili tufanye nao kazi. Nataka Nachingwea ibadilike, zile barabara zote tutazijenga kama tulivyoahidi kwenye ilani yetu,” amesema.

Baada ya Rais Dk. Magufuli kuzungumza na wananchi hao, Majaliwa aliwasisitiza wakazi hao wahakikishe kesho wanapiga kura zote za ndiyo kwa mgombea urais, wabunge na madiwani wa CCM ili wapate ushindi wa kishindo.

“Kesho asubuhi, kila mmoja na kadi yake, nenda kapige kura. Wako waliojipanga kununua kadi za wapigakura ili kutunyima ushindi. Kura yako ina thamani sana kuliko hiyo elfu tano atakayokupa. Usikubali kupoteza kura yako.”

Wakati huo huo, mbunge mteule wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye alipopewa nafasi kumuombea kura Dk. Magufuli alisema ana imani kwamba ushindi wa CCM uko dhahiri kwani hapo Nachingwea wakazi wake ni karibu 100,000 lakini wanaCCM peke yake ni 86,000.

“Hawa wanataka kushindana na CCM, sasa hao watashindaje? Kati ya majimbo zaidi ya 200 hapa nchini, tayari tuna majimbo 28 ambayo wagombea wake wamepita bila kupingwa. Tukienda kwenye urais, tuna wapiga kura milioni 29 na kati yao, milioni 18 ni wanaCCM. Je bado wana nafasi ya kushinda? Watapitia wapi?” alihoji.

Aliwataka wakazi hao waache ushabiki wa kisiasa na wajifunze kutoka nchi jirani ambayo wananchi wake walipata maafa baada ya uchaguzi na wagombea wakabakia na makundi