*Mji wa Kayanga kupata barabara za lami, imo
ya Murushaka – Murongo
SERIKALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imetumia sh.
bilioni 1.8 kujenga majengo mbalimbali ya hospitali ya Wilaya ya Karagwe ambayo
yamekamilika kwa asilimia 98.
Hayo yamesemwa jana (Jumanne, Septemba 29, 2020) na
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Kayanga, katika mkutano
uliofanyika kwenye uwanja wa Changarawe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera.
Akielezea ujenzi wa vituo vya afya kwenye wilaya
hiyo, Majaliwa alisema sh. milioni 900 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya vituo vya afya ambapo kati ya hizo, sh.
milioni 500 zimetumika wa majengo ya kituo cha afya cha Kayanga ambapo kituo
hicho kimekamilika na kinatoa huduma.
"Shilingi milioni 400 zimetumika kwa ujenzi wa
majengo ya kituo cha afya cha Nyakayanja na ujenzi umekamilika. Pia shilingi
bilioni 2.5 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi
huku fedha za dawa kwa mwezi zilikuwa ni wastani wa shilingi milioni 53,”
alisema.
Akielezea uboreshaji wa miundombinu kwenye wilaya
hiyo, Majaliwa alisema ukurasa wa 74-76 wa Ilani ya uchaguzi ya CCM, unaelezea
mpango wa serikali kuanza ujenzi mpya (km 6,006.04) na ukarabati wa barabara
kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Mugakorongo - Kigarama - Murongo yenye
urefu wa km 105.
“Ilani yetu imeenda mbele zaidi na kuelezea
mpango wa kukamilisha/kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina (km 7,542.75)
barabara za mikoa kadhaa ikiwemo barabara ya Murushaka – Murongo yenye km
125.”
Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura
mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi
mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, mgombea udiwani wa kata
ya Kayanga na wagombea wa CCM wa kata za wilaya hiyo.
Alisema sh. bilioni 1.4 zimetolewa kupitia
Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya kufungua barabara
mpya, matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, muda maalum na
makalvati.
Alisema kati ya hizo, sh. milioni 585 zimetolewa
kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi na baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa
kazi ni ukarabati katika barabara ya Nyakagoyagoye-Karongoambao uligharimu
sh. milioni 31.
Akielezea ukarabati uliofanywa, alisema sh. milioni
19 zimetumika katika barabara ya Kanyabuleza-Runyaga; sh. milioni 14
zimetumika na katika barabara ya Mato-Karehe; sh. milioni 23 zimetumika
katika barabara ya Kihanga - Rwabitembe – Mshabaiguru, sh. milioni 16
zimetumika katika barabara yaNyakahanga – Kamahungu, sh. milioni 16
zimetumika katika barabara ya Kishoju – Bujuruga na sh. milioni 23
zimetumika katika barabara ya Igurwa-Kibona-Nyakahita.
Alizitaja barabara nyingine zilizofanyiwa ukarabati
kuwa ni Katoju-Ihembe – Bisheshe iliyogharimu sh. milioni 98, barabara ya Kanyabuleza
Jct-Makabulini iliyotumia sh. milioni 69, barabara ya KDVTC
FADECO iliyotumia sh. milioni 73, barabara ya AMRI – CLASIC
iliyogharimu sh. milioni 38 na barabara ya Rukore – Chanikailiyotumia sh.
milioni 115.
Alisema TARURA ilifanya matengenezo ya madaraja na
makalvati katika barabara za Katoju- Rugu - Ruhita (sh. milioni
17), Igurwa-Nyakashozi-Rwentuhe (sh. milioni13),Rukore -
Chanika (sh. milioni 12),Rubale - Kibogoizi (sh. milioni 6)
na barabara ya Kasheshe - Rubare (sh. milioni 7).
“Shilingi milioni 124 zimetumika kwa ajili ya
matengenezo maalum katika barabara za Kajunguti - Rubare -
Misha (km. 9), Nyabiyonza-Kafunjo(km. 6), Kibaoni
Nyabiyonza Sec - Kakuraijo (km. 3.15), Nyakakika - Kandegesho (km.5),
Lukole - Kigarama, Lukoyoyo – Kantabire -Nyakasimbi na Ahamulama – Busecha,”
alisema.

No comments:
Post a Comment